RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

USIONE HAYA KUMUIMBIA MUNGU..SHAURI YAKO..TAMBUA YA KUWA MUNGU WETU NI MUNGU WA SIFA

Mungu wetu ni Mungu wa sifa, na kama Mungu wetu ni Mungu wa sifa basi huu ni wakati wa kumpa sifa zake kwa njia ya uimbaji. haijalishi sauti yako iko nje ya ufunguo au ndani ya ufunguo, una haki mbele za Mungu kupaza sauti yako na kumuimbia Mungu wa mbinguni. Usiwe mtu wa kushangaa unapoona wenzako wanamsifu Mungu kwa kuimba. Tumechoka na kusikia watu wakiiimba na sisi kubaki tunashangaa kama vile hatuna sauti za kumuimbia Mungu. Rafiki yangu anza sasa kupenda kumuimbia Mungu, unapoona kanisani au mahali popote pale watu wamekusanyika kwaajili ya sifa ninakuomba ujichanganye nao kwani ndani ya sifa kuna mpennyo mkubwa sana wa kupokea baraka za Mungu

Kuna jambo ambalo mimi binafsi huwa linaniboa sana kwa waimbaji wa nyimbo za Injili na huwa najiuliza sana ni kwanini...? Utamkuta mwimbaji amefanya vizuri katika albamu ya kwanza, napokuja kutoa albamu ya pili inakuwa haina mvuto bali ni ya kawaida..Rumafrica inafanya jitihada ya kutafuta baadhi ya waimbaji na kufanya nao mahojiano

TUONE WENZETU WALIVYOKUWA WAKISIFU KATIKA KANISA LA RGC MIRACLE CENTER TABATA CHANG'OMBE KWA MTUME PETER NYAGA.
Kushoto ni Mama Mchungaji Anna Nyaga wa kanisa laRGC akimpongeza Neema Gasper wakati wa kipindi cha sifa
Neema akiachia sauti yake itumike ipasavyo kwa utukufu wa Mungu
\\\\








Comments