RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

ILE SIKU YA KULA WALI NA VINYWAJI KATIKA HARUSI YA ROSE MUSHI NA SHABOKA JR IMEKALIBIA

Zikiwa zimesalia siku 60 kufikia siku kubwa kabisa katika maisha yangu, siku ya Harusi yangu 29 JUNE 2014. Ninamshukuru kila mmoja wenu aliyenipigia simu au kunitumia ujumbe kunipongeza kuniombea, kunishauri na kuniunga mkono kifedha ili tu kufanikisha mchakato huu. Namna mlivyoonyesha kufurahi pamoja nasi na kutuunga mkono mmetutia moyo na kutuonyesha mnakubaliana na uamuzi tuliouchukua. Binafsi Nimeguswa na moyo wa shirika ambao mnanionesha sehemu mbalimbali.

Wengine kwa sababu ya umbali lakini wangetamani kufanya kitu kwaajili ya siku hiyo, nimeona nisiwanyime nafasi ya Baraka ya kusimama pamoja nami katika wakati huu muhimu katika maisha yangu. Hivyo nimeamua kuweka namba za simu hapa ili kwa wewe uliyembali uweze kushiriki vile Mungu ameweka moyoni mwako kufanya. Usijione mnyonge wala usione ni kidogo kwani Yesu alitumia Mikate mitano na samaki wawili wa yule kijana katika Yohana 6:1-13 kulisha watu zaidi ya elfu tano. Vipi kama kijana angejidharau kwa kuona ana mikate mitano tu na watu ni maelfu?

Mungu tunayemtumikia awabariki na kuwaongeza, Nashukuru sana sana sana, zaidi ya yote tuendelee kuinuana katika maombi ili kusudi la Mungu litimie kwa mafanikio. Unaweza kuwasiliana na namba hizi kwa taarifa zaidi, kuwasilisha mchango wako au kutuombea.
- 0753 310 587
- 0715 310 587
- 0784 310 587.


JEHOVA AKUBARIKI NA KUKUINUA with Rose Mushi

Comments