RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

MASANJA MKANDAMIZAJI AWASHA MOTO KATIKA MKUTANO ULIOFANYIKA IRINGA KWA MCHUNGAJI CHACHA

Mchungaji Mtarajiwa Emmanuel Mgaya (Masanja Mkandamizaji hivi juzijuzi aliweka historia ya mwaka katika mkutano uliofanyika mkoani Iringa kwa ambao uliandaliwa na Mchungaji Chacha. Watu walikuwa wengi sana waliofika katika mkutano kutookana na uwepo wa mwigizaji na mchekeshaji Masanja Mkandamizaji. Watu walipokea ujumbe kwa njia ya uimbaji kutoka kwa Masanja na pia Neno la Mungu kutoka kwa Mchungaji Chacha.


Emmanuel Mgaya (Masanja Mkandamizaji)

Masanja anategemea kuhudumu katika mkutano utakaofanyika Morogoro kwa mwinjilisti Jailos Maloda ambapo Mtume Nyaga wa kanisa la RGC Tabata Chang'ombe hapa Dar es Salaama atahubiri. Mkutano huu unaenda kwa jina la MOROGORO YOTE KWA YESU. Kutakuwa na waimbaji mbalimbali kama utakavyowaona katika tangazo la hapo chini.

Masanja Mkandamizaji akifanya yale anayotakiwa kuyafanya kwa utukufu wa Mungu mkoani Iringa

Masanja Mkandamizaji akifanya yale anayotakiwa kuyafanya kwa utukufu wa Mungu mkoani Iringa






Comments