RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

NDOA HII NI YA KUIGWA - BONY MAGUPA NA MKE WAKE JESSICA MAGUPA

Hawa jamaa ukiwaona unaweza kufikiri ni mtu na dada yake au rafiki yake, utasahau ya kwamba ni wanandoa jinsi wanavyoishi na hasa wanavyokuwa kitaa. Nimeona ndoa lakini hii ni kiboko. Nilkuwa najiuliza, au kwa sababu wote wako katika maswala ya media nini ndio maana interest zao zinaendana. Nadhani unajua ya kwamba Jessica Honore Magupa ni mwimbaji wa nyimbo za injili na mume wake Bony Magupa ni Mtangazaji wa redio Praise Power na wote wawili ni watu wa kupiga majingo maredio na hasa Praise Power na Clouds FM. Kuna sehemu wanatofautiana katika kazi, Bony Magupa ni MC wakati Jessica Honore Magupa ni mwimbaji wa nyimbo za injili na mjasiliamali..Ila hawa jamaa kiboko.


Unajua Bony alimpataje Jessica Honore na mpaka sasa wanaitwa wanandoa? Siku moja Jessica alitia timu Praise Power kupeleka nyimbo yake radioni na alipofika pale ghafla Mungu akawagonganisha na Bony Magupa na kuanzia hapo Bony hakuweza kuachia uzi na leo wanaitwa wanandoa.

Poa wangu ni hayo...
Rulea Sanga

Comments