RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

RULEA SANGA APONA JINO BAADA YA KUTUMIA MAJI YA UPAKO YA TB JOSHUA


Baada ya kusumbuliwa na jino kwa muda mrefu, siku moja niliamua kumuomba Mungu kabla ya kutumia maji ya upako ya TB Joshua. Nilipomaliza kuomba nikaendelea na mishemishe zangu za kawaida. Ilipofika jioni jino langu likaanza mabo yake, nilijisikia maumivu makubwa sana yakiambatanisha na jicho na kichwa. Muda ulivyokuwa ukisonga mbele maumivu nayo yakazidi kuwa makali. Niliingia chumbani na kuchungulia jino langu katika kioo.

Rulea Sanga


Jino langu nililionekana kuchimbika sana, nirudi sebuleni na kuvuta kiboko ya yote yaani maji ya Upako ya TB Joshua na kupulizia katika jino langu, lakini maumivu yakazidi kuongezeka. Nilipiga goti huku nikiwa nimeinua mkono wangu wa kulia nikiomba Mungu anisaidia. Mhh...baada ya kuona hali inazidi niliamua kukata maombi na kujilaaza huku nikigalagala sana. Baada ya muda fulani nikasikia sauti ikiniambia nichukue maji ya upako na nilalie kichwani, niliamua kufanya hivyo. Jamani Mungu wa TB Joshua mwaacheni aitwe Mungu, nilipata usingizi wa ajabu na kulipokucha nikajisikia ile hali ya maumivu imepungua. Siku zilivyokuwa zikizidi kusonga maumivu yakawa yanafyata mkia na kuondoka katika mwili wangu. Mpaka sasa naandikaushuhuda huu niko fiti na ninapiga misosi kama soina akili sana.

Ninakushukuru sana Mungu wangu na Mungu wa TB Joshua

Wenu katika Bwana
Rulea Sanga
+255 715 851523

Comments