RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

ALIYEKUWA MUME WA MONALISA NA MWONGOZA FILAMU TANZANIA MAREHEMU TYSON AFARIKI DUNIA KWA AJALI YA GARI WAKATI WAKITOKA MKOANI DODOMA

PICHA ZA GARI ALILOKUWEMO

Marehemu Geogre Tyson pichani hapa alikuwa yupo kijiji cha Chilonwa Chamwino kwenye utoaji wa madawati katika shule ya msingi Chaula iliyopo Dodoma. Baada ya kumaliza shughuli hii huku akiwa kama producer wa The Mboni Show mauti yalimkuta majira ya saa 12 jioni masaa 4 tu toka tuanze safari ya kurudi Dar es Salaam maeneo fulani hivi kama unataka kukaribia GAIRO mjini.

Katika gari hilo walikuwa watu 8 ila yeye pekee ndio aliyepoteza maisha na wengine kupata majiraha mwilini pamoja na dereva wa gari hilo. Kwa sasa mwili wa marehemu umehifadhiwa Morogoro katika hospital ya mkoa Morogoro, baadae asubuhi mwili utaanza safari ya kuelekea Dar es Salaam.








Kweli ajuae mwisho wetu ni Mungu pekee. Tunaishi kama vile tunajua maisha yetu yataisha lini kumbe tunajidanganya. Haya matukio yote ni kwa ajili yetu kuamka na kujifunza kitu. Tumrudieni Mungu, tuungame dhambi zetu maana hakuna ajuae siku wala saa yake itakuwa lini. R.I.P Tyson na wote mliotutangulia.

Picha zote kutoka DJ Choka Music.

Comments