RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

KANISA LA WASABATO MZIZIMA LASAIDIA WATU WASIOJIWEZA




Chama ya kinachowaunganisha wanaume na wanawake wa Kanisa la Waadventista Wa Sabato AMO DORKAS katika kanisa la Waadventista Wa Sabato Mzizima jijini Dar es salaam wametembelea kituo cha watu wasiojiweza cha Nunge kilichoko jijini Dar es salaam na kutoa misaada ya kijamii na kiroho.

Kituo hicho ambacho kipo chini ya Serikali kina idadi ya wazee 37, watoto wanaoishi na ulemavu wa kusikia 23 na watoto yatima.

Kwa mujibu wa blog ya Networked chini ya mtangazaji Maduhu imeandika kwamba sambamba na kutoa huduma ya neno la MUNGU pia wametoa msaada wa mavazi,mchele, sabuni, na unga wa lishe na dawa kwa Wagonjwa.

Kwa upande wake kiongozi wa mawasiliano wa kanisa la mzizima Kapesa Manyoni ambaye pia alikuwa mkuu wa msafara ameiomba jamii kuonesha upendo kwa watu wasiojiweza na kwamba wao kama kanisa wataendelea kufanya hivyo.

Kwa upande wake Afisa Msaidizi wa Kituo hicho Bwana Mosses Gunza ameshukuru kwa kupokea msaada huo na kusema kuwa ni kuonesha upendo wa Mungu kwa watu wasiojiweza kwani Hawakupenda kuwa hivyo.

Wazee hao pamoja na watoto yatima wameiomba serikali kuweka utaratibu wa kuwahisha misaada ili iweze kuwafikia kwa wakati hali ambayo itasaidia upatikanaji wa mahitaji kwa urahisi.

Comments