RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

TUZIDI KUMUOMBEA DEBORA JOHN HALI YAKE SIO NZURI. SEMA NENO JUU YAKE

Tunahitajika kumuombea ndugu yetu na rafiki yetu Debora John kwa wakati huu anaopitia. Hiki ni kipindi kigumu sana kwake kwania anateseka sana na maumivu makali. Habari zinasema Debora John Saidi ambaye hali yake inaelezwa kwamba si nzuri nasasa yuko chumba cha upasuaji hospitali ya Mwananyamala kuondolewa uvimbe mkubwa tumboni ambao umesababisha alie kwa maumivu makali.

Upasuaji wa kutoa uvimbe huo ulitarajiwa kufanyika kesho, lakini kutokana na maumivu pamoja na kilio kutoka kwa mwimbaji huyo imebidi kupelekwa chumba cha upasuaji mchana huu. Ambapo mchana wa leo baadhi ya waimbaji wenzake akiwemo Joshua Makondeko, Tumaini Njole walifika hospitalini hapo kumjulia hali.

Debora akilishwa kabla ya kupelekwa chumba cha upasuaji.

Mungu akuponye Debora.



Joshua Makondeko akimnywesha maji Debora.

Comments