RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

FURAHA ISAYA KUFANYA UZINDUZI WA ALBAMU YAKE YA "NITASEMA NDIYO KWA BWANA" LIVE

Inafurahisha kuona sasa vijana wa Yesu wanafanya kazi ya Mungu kwa viwango vingine bila hata ya kuogopa changamoto zinazowazunguka. Hii tunasema ni kuthubutu bila ya kuangalia nani anasema nini, bali ni kumuangalia Jehova.

Furaha Isaya ni mwimbaji wa nyimbo za injili ambaye kwa sasa Mungu amemuweka katika viwango vingine vya kimuziki. Mungu ameweza kumsaidia na kumuwezesha kumaliza albamu yake ya NITASEMA NDIYO KWA BWANA" akiwa amewashilikisha baadhi ya waimbaji kama vile John Shabani.

Mungu hakuishia hapo, pia amempa kibali cha kuweza kuzindua albamu yake LIVE katika ukumbi wa URAFIKI SOCIAL HALL ulipo Sinza Legho. Tamasha hili litaanza saa 6 mchana hadi saa 12 jioni na kutakuwa na kiingilio cha Tshs. 2,000 tu.

Tamasha hili limegubikwa na waimbaji wengi sana, baadhi yao ni Atosha Kissava, Ambwene Mwasongwe, Madam Ruti, Edson Mwasabwite, Neema Gasper, Masanja Mkandamizaji, Sarah Mvungi, Joshua Makondeko, Mercy Kitundu, Mess Chengula, Stella Joel, Emmanuel Mabisa, Grace Rwegasha, Enock Jonas, Marry Mgogo, Silas Mbise, Julieth Dougras, John Shabani, Jerry Mtumishi, Hondwa Mathias, Petro, Emmanuel Peter, Danniel Safari, Leah Amos, Margreth Sembuche, n.k




Comments