
Hapo jana kanisa la Hillsong tawi linalotumia ukumbi maarufu wa Dominion Theatre uliopo makutano ya barabara ya Tottenham Court Road na Oxford katikati ya jiji la London, ilikuwa siku yao ya mwisho kuutumia ukumbi huo ambao unafungwa kwa matengenezo na kufunguliwa tena mwezi octoba mwaka huu.
Kupitia katika ibada ya jana, waumini wanaoshiriki katika ukumbi huo walipata nafasi ya kusikiliza mahubiri kutoka kwa mchungaji kijana Dan Blythe aliyehubiri kuhusiana na sifa kwamba ni lazima itoke ndani ya moyo na sio nje kama baadhi ya watu wanavyodhani, somo ambalo aliweza kulifafanua vyema akiambatanisha na vichekesho vya hapa na pale kufanya waumini kufuatana naye mpaka mwisho.
Kanisa hilo linatarajiwa kuhamia kwenye ukumbi wa The New London Theatre kuanzia jumapili ijayo, huku likitarajiwa kuongeza ibada nyingine na kufanya kuwa na jumla ya ibada tano kila jumapili kutoka ibada nne walizozoea kuendesha kila jumapili. Kurejea kwao mwezi wa kumi katika ukumbi wa Dominion kutawapa uhuru wa kutumia ukumbi huo kwa muda wautakao kwa siku za jumapili tofauti na awali ambapo mara baada ya ibada walihitajika kuondoa vifaa vyao haraka ili kupisha burudani nyingine.

Watu wakitoka ukumbini baada ya ibada.

Watu wakiingia ukumbini hapo ikiwa ni siku ya mwisho kupisha matengenezo.

Kilikuwa kipindi safi sana cha uimbaji.
SOMA ZAIDI KWA KUBOFYA "READ MORE" HAPO CHIINI













Comments