RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

JULIETH DOUGRAS AFUNGUKA NA KUELEZEA KILE ALICHOJIFUNZA KATIKA UZINDUZI WA ALBAMU YA FUARA ISAYA


Julieth Dougras ni mwimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania ambaye anafanya vizuri sana kwa uimbaji. Siku ya tamasha la Furaha Isaya alishiriki kama mwimbaji wa kuitikia katika tamasha lililofanyika LIVE katika ukumbi wa Social Hall Sinza Legho hapa Dar es Salaam Tanzania. Mwimbaji huyu ambaye ndio kwanza ameanza huduma yake ya uimbaji, amefanyika baraka kwa walio wengi na walioweza kusikia nyimbo zake.
Julith Dougras

Mbali na kushiriki tamasha hili pia Mungu amemuwezesha kuwa na albamu yake ya "U Mtakatifu" ambayo inafanya vizuri sana na watu wengi wameweza kupokea majibu yao kwa njia ya uimbaji wa dada Julieth Dougras.

Kuna mambo mengi ameweza kuongea na Rumafrica kuhusiana na tamasha la kipekee la dada Furaha Isaya lililofanyika hivi karibuni. Kuna mengi amejifunza kama mwimbaji chipukizi ambayo anasema kwake yatabadilisha maisha yake kama atayafuata na kuzingatia. Tumskilize kile alichokiongea.




Comments