RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

MH. JANUARY MAKAMBA AZUNGUMZA NA WANAMUZIKI WA INJILI TANZANIA SIKU YA LEO


Chama Cha Muziki wa Injili Tanzania siku ya leo kiliada mkutano wa wanamuziki wa Injili Tanzania katika hoteli ya Wanyama Sinza Mori hapa Dar es Salaam. Katika mkutano huo mgeni rasmi alikuwa Naibu Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia, Mh. Januari Makamba ambaye aliongozana na mdogo wake Latifa Makamba, aliweza kuongea mengi juu ya wanamuziki wa Injili Tanzania. Msafara huu uliambatana na viongozi kutoka COSOTA, TRA na BASATA ambao waliweza kuongea mengi kuhusiana na taratibu, sheria na vigezo vya mwanamuziki kuwa navyo ili aweze kutambulika kuwa mwamamuziki na ana haki zake.

Mh. Januari Makamba

Mh. Januari Makamba aliweza kutoa hutuba ndefu yenye ufasaha kwa wanamuziki wa Injili Tanzania. Hotuba yake ilikuwa na matumaini kwa wanamuziki na iliweza kuwafurahisha sana wanamuziki hawa hasa pale alipoweza kutoa ahadi zake za kukisaidia Chama Cha Muziki wa Injili Tanzania ikiwemo kuwa mlezi wa chama hicho na kuwaahidi kuchangia katika kufanikisha zoezi la kuwa na Channel ya TV ya waimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania. Aliomba sana wanamuziki kuwa na nguvu za bidii za kuweza kufanikisha yale yote yanayowazunguka na wasibweteke wakisubiria kusaidiwa.


KIPINDI CHA MGENI RASMI MH. JANUARI MAKAMBA KUWASILI KATIKA UKUMBI WA WANYAMA SINZA MORI KWA MKUTANO
 Baadhi ya viongozi wa COSOTA, BASATA, CHAMUITA na TRA wakiwa tayari kumpokea Mh. Januari Makamba
 Kutoka kushoto ni Mch. Lucy Wilson, Christina shusho, George Mpera, Joshua Makondeko wakisubiri mgeni rasmi kuingia

Rais wa CHAMUITA Addo November akifunga mlango wa gari la Mh. Janauri Makmba baada ya kushuka

Mh. Januari Makamba akisalimiana na baadhi ya viongozi wa COSOTA, BASATA, CHAMUITA na TRA baada ya kuwasili katika hoteli ya Wanyama Sinza Mori.

Mh. Januari Makamba akiongea na Christina Shusho kabla ya hotuba yake kuitoa

KIPINDI CHA KUTAMBULISHA

Kiongozi wa CHAMUITA John Shabani ambaye kwa siku hii alikuwa MC aliweza kuwatambulisha baadhi ya watu waliofika katika mkutano huu

Kiongozi CHAMUITA  kutoka Morogoro akikabidhi MIC baada ya kujitambulisha


Muwakilishi kutoka ATN akijitambulisha
 Kushoto ni mtangazaji wa Praise Power Radio, Erick Brighton
 Kulia ni mwimbaji Lugano Mwiganege
 Kulia ni Annie Mwasomola akiwa na Mzee Kitime
 Jessica Honore wa kili kutoka kulia akiwa makini
 Viongozi wa CHAMUITA kutoka Morogoro na ni waimbaji wa nyimbo za Injili
 Wa kwanza kulia ni mwimbaji Mkuruta Nestor



KIPINDI CHA KUFUNGUA KIKAO KWA MAOMBI

 Mh. Janauari Makamba akiwa katika maombi

KIPINDI CHA MWALIKWA MNENAJI PROF. COSTA MAHALUM KUTOA HUTUBA YAKE
Mbunge wa Bunge la Katiba Mh. Prof. Costal Mahalu akieleza machache kwa waliohudhuria mkutano huo.



KIPINDI CHA MGENI RASMI NA WANAMUZIKI KUSIKIA MACHACHE KUTOKA KWA VIONGOZI WA COSOTA, TRA, CHAMUITA na BASATA
 Kushoto ni Rais wa CHAMUITA Bw. Addo Novemba


KIPINDI CHA MASWALI NA MAJIBU KUTOKA KWA WANAMUZIKI WA INJILI



 Kiongozi kutoka BASATA akijibu maswali
 Kiongozi kutoka TRA akijibu swali kutoka kwa wanamuziki
 Kiongozi kutoka BASATA akijibu maswali kutoka kwa wanamuziki
 Mtangazaji wa Praise Power George Mpera akiuliza swali kwa viongozi waalikwa
 Kulia ni Grace Rwegasha akisikiliza kwa makini
 John Shabani akihakikisha kila kitu kinaenda sawa wakati watumishi wa Mungu wakiuliza maswali.
 Mzee Makassy anaye aliweza kuchangia maada zilizokuwa zikiendelea katika mkutano huu.

KIPINDI CHA MH. JANUARI MAKAMBA KUTOA HOTUBA KWA WANAMUZIKI WA INJILI TANZANIA

Upendo Kilahiro kulia akiwa makini sana kusikiliza yanayozungumzwa na Mheshimiwa

KIPINDI CHA KUPIGA PICHA ZA PAMOJA KILIFIKA


Mzee wa matukio, Rulea Sanga wa tatu kutoka kushoto hakuwa mbali katika picha ya pamoja



Kutoka kulia ni John Shabani, Upendo Kilahiro, Addo Novemba na Mh. Januari Makamba


Wa tatu kutoka kushoto ni bloga Rulea Sanga

Wa tatu kutoka kushoto ni bloga Rulea Sanga



Comments