RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA INATOA POLE KWA MWIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI BAHATI BUKUKU KWA AJALI MBAYA ALIYOPATA

Rumafrica imepokea taarifa za ajali ya gari ya mtumishi wa Mungu Bahati Bukuku kwa masikitiko makubwa sana. Taarifa hii hakuwa nzuri kabisa masikino mwetu, ilileta majonzi na huzuni kwetu. Tulipota habari hizi kutoka kwa mwimbaji wa nyimbo za Injili Catherine Kyambika katika mkutano wa wanamuziki wa nyimbo za Injili ambao ulifanyika 26.07.2014 katika hotel ya Wanyama na mgeni rasmi alikuwa Mh. Januari Makamba, waimbaji waliweza kushtushwa sana na wengine kuwa na maswali mengi sana vichwani mwao,

Dada Catherine Kyambiki aliweza kututaarifu ya kwamba dada yetu Bahati Bukuku amevunja kiuno na yuko hospitalini kwa matibau, hakiki hii haikuwa taarifa nzuri kwetu,

Sasa, kama watumishi wa Mungu tunalazimika sasa kuomba juu ya dada yetu Bahati Bukuku ili aweze kupona na aendelee na kazi ya Bwana wetu Yesu Kristo. Katika maombi yako unaombwa sana kumuombea afya njema dada Bahati Bukuku. Usiwe mbinafsi wa maombi katika kipindi hiki kigumu kwa wanamuziki wa wadau wa muziki wa Injili duniani.

Wenu katika Bwana
Rulea Sanga
RUMAFRICA FOR ALL NATIONS

Comments