RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

GAZUKO ANAYESUBIRI KUKWEA PIPA KWENDA UINGEREZA KWENYE TUZO ZA AFRICA GOSPEL MUSIC AWARDS AFUNGUKA NA KUTOA SIRI YA JINA LAKE LA GAZUKO NA SIRI YA YEYE KUCHAGULIWA..MSIKILIZE AKIONGEA NA RUMAFRICA

Hivi karibuni mwana Hipo Hop wa Gospo Tanzania GAZUKO ambaye amechaguliwa katika mashindano ya tuzo za kimataifa za Africa Gospel Musics Awaards 2014 hungo unyamwezini aliweza kuongea na RUMAFRICA mengi, Mwanaharakati huyu ambaye kwa sasa ana kilio kikubwa kutoka kwako cha kumpigia kura ili ashinde katika category yake ambayo ina watu kama 15, alizungumza mengi na kutoa siri ya jina lake la GAZUKO na pia aliweza kuzungumzia sifa za mwimbaji kuweza kufahamika kimataifa kama yeye alivyofahamika na mataifa makubwa na kuona thamani ya kazi yake.
Kuna baadhi ya mambo ambayo kama GAZUKO aliweza kuyatoa moyoni mwake ambayo yamekuwa kikwazo kibwa sana katika harakati za kumtangaza huyu YESU KRISTO kutoka kwa watu mabalimbali wanaotaka kumzibia hii fursa aliyopata.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhqv-TjLI2CoLAoDdZ7vAFJLXRvfMG2Z5cOLYwh5Tqsyuqieyv5F8iAHd4hAIgErrurLD23wPHZ-lVkClPBiTbpT1IRKIHmDv-ftETVRP-95-Sja43m8bg_ymxGJkJu8Vi-p3i2fK5Qap8/s1600/734429_531811490246582_1057259145_n.jpg
Mwanaharakati wa HIP HOP GAZUKO akiwa katika moja ya mitaa yake.

GAZUKO kwa asiyemjua huwezi kumwelewa ila kijana ambaye ana uchungu wa maisha ya hapa duniani na ana hamu kubwa ya kuonana na Mungu na kurahia ile paradiso na ndio maana anajitahidi sana kufanya awezalo kwa kutumia mali zake na akili zake ili kazi ya Bwana iwe katika viwango tofauti kabisa. Kutokana na juhudi hizo ndio maana Mungu ameweza mkumuinua na kumtambulisha kimataifa.

MSIKILIZE MWANAHARAKATI GAZUKO AKIONGEA NA RUMAFRICA HIVI KARIBUNI


SIKILIZA BAADHI YA KAZI ZA GAZUKO


HAYA NI MAJINA YA WASHIRIKI WA CATEGORY AMBAYO YUMO GAZUKO

Afro Rap Artiste of the Year

1. MOG (Netherlands)
2. SI Unit (Ghana)
3. Cjay (South Africa)
4. Pompi (Zambia)
5. VKP (Kenya)
6. Kris Eeh Baba (Kenya)
7. Gaise (Nigeria)
8. Provabs (Nigeria)
9. Andrew Bello (UK)
10. Lyrical Soldier (UK)
11. Royal Priesthood (Ghana)
12. Dolly P (UK)
13. X-Caliber (Botswana)
14. Gazuko (Tanzania)
15. David Kalilani (Malawi)

UKITAKA  KUMPIGIA KURA GAZUKO BONYEZA HAPA: GAZUKO

Comments