RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

JENIFFER KYAKA ASHEREKEA NA WATOTO YATIMA KATIKA BIRTDAY PARTY YAKE SIKU YA JANA

Mwigizaji wa filamu Tanzania na Mkurugenzi wa J-Film 4 Life, Jennifer Kyaka ()dama) siku ya jana ilikuwa ni siku yake ya kipekee ya kuzaliwa kwake. Katika siku hii ambayo alikuwa anamshukuru Mungu kwa kumuwezesha kutimiza mwaka mwingine, aliweza kuwaalika watoto yatima pamoja na walezi wanao walea kusherekea pamoja na kumshukuru Mungu.

Mkurugenzi wa J-Film 4 Life, Jeniffer Kyaka (Odama)

Odama aliweza kugawa zawadi ya vyakula, vinywaji na mavazi kwa watoto hao pamoja na nguo kwa walezi wanaowalea watoto hao. Watoto walionyesha moyo wa shukrani sana kwa Odama kwa upendo na huruma alionayo na jinsi alivyoweza kufurahi nao. Watoto yatima walipata muda wa kucheza muziki, kula na kunywa na msanii huyo pamoja.

Katika sherehe hiyo kulikuwa na wasanii wa Bongo movie wengi sana wakiwa wameongozana na Rais wao Steve Nyerere, baadhi yao ni Kajala, Lamata, Rhoda, Stamford, Ashura (dada wa make up), Issa, Malick, Farid Uwezo, Johari, Mlela, Jada, Bi Mwenda, Dyness (madau wa Bongo Movie)

KAtika sherehe hiyo pia alikuwepo baba mzazi wa Odama na familia yake yote ambao walifika kwaajili ya kumuunga mkono na kuhakikisha sherehe inakuwa ni ya baraka kwa wote waliofika siku hiyo.

Hakika watu walifurahi sana na ilionyesha ni jinsi gani watu wanamkubali Odama na amefanyika baraka kwa walio wengi kwa upendo wake na huruma yake. Odama ambaye anaonekana kukubalika katika jamii kwa kazi zake na jinsi anavyojiheshimu kwa kila idara siku ya jana alionyesha upendo wa dhati kwa kujishusha na kuonekana ni mtu wa kawaida tofauti na watu wengine ambao wakiwa na jina kubwa wanapandisha mabega yao na kujivuna.

Mbali na uigizaji, Odama pia ni mkurugenzi wa kampuni yake ya J-FILM  4 LiFE ambayo inahusika na kuandaa filamu na pia inahusika na mambo mengine ambayo siku moja Rumafrica itakuletea baada ya kufanya mahojiano na msanii huyu.

Sasa ngoja tuone baadhi ya matukio ya siku ya jana katika ukumbi wa Vijana hall uliopo Kinondoni Dar es Salaam Tanzania.
KIPINDI CHA KUPIGA CHINI YA KAPETI JEKUNDU

Msanii wa Bongo Movie Sandra

KIPINDI CHA KUPATA CHAKULA CHA JIONI
 Baadhi ya watoto yatima wakipata chakula cha jioni

watoto yatima wakipakuliwa chakula cha jioni

Baadhi ya watoto yatima walioalikwa na Jeniffer Kyaka (Odama) wakipata chakula cha jioni na vinywaji kama unavyoona
 Mwalimu wa watoto yatima akipata chakul
 Huyu ni msanii wa Bongo Movie aliyecheza filamu ya Kibajaji
 Msanii wa Bongo Movie Rhoda akipata chakula cha jioni
 Mdau wa Bongo Movie Dai akiongozana na msanii maarufu Kajala wakijipatia msosi wa jioni

 Camera Man Farid Uwezo akipata msosi wa jioni

 Mdogo wake na Odama , Joan akijipatia msosi wa jioni
 Sandra wa Bongo Movie akijipatia msosi wa jioni
 Mdogo wake na Odama, George akipata chakula cha jioni
 Baadhi ya wasanii wa Bongo Movie wakipiga story huku wakipata cjhakula maridadi pamoja na yatima
 George Kyaka (wa tatu kutooka kulia) na marafiki zake wakipata chakula cha jioni

KIPINDI CHA BURUDANI
Dada huyu alikonga mioyo ya watu wengi pale tu alipoanza kucheza, aliwafurahisha watu wengi sana na ikafika watu wakaanza kutupia manoti kwa kumpongeza

 Kajala wa Bongo Movie akimtunza dada huyu kwa uchezaji wake






Comments