RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

KUJIFUNZA KUIMBA OPERA NA KUWA NA SAUTI NZURI

MWIMBAJI amesimama wima akiwa mtulivu, ameinua kichwa na kifua, paji la uso wake limetulia, nayo midomo na kinywa chake vimetulia pia. Baada ya muziki kupigwa kwa kipindi kifupi, mwimbaji anaanza kuimba wimbo ambao umekuwa ukitazamiwa kwa hamu. Inaonekana anaimba kwa mtiririko bila jitihada yoyote hivi kwamba utafikiri si yeye anayeimba. Anapomaliza tu kuimba, makofi yanafuata!
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiCWGUeY-BOljUdpHm9qCACE3Tju36-cVHKQgMmiQ5FRUE_1Z2D4qOVrhFMkKyapv8u_y-k_yyNog29noRPjgDNI9-tvdLmbAJUeU7Z10TiLKPnCRhAtimN44JdukRINUV4vo3X4VowzIrH/s640/r7.jpg
Upendo Kilahiro kutoka Tanzania

Opera ni drama inayoigizwa na wahusika wanaoimba wakifuatana na muziki wa okestra. Je, wewe hufurahia opera? Umewahi kuhudhuria maonyesho ya opera? Unafikiri ni nini kinachomwezesha mwimbaji wa opera kuwa na sauti tamu?

Sauti Ni Ala ya Muziki
Sauti ni zawadi nzuri sana tuliyopewa na Mungu, na si ajabu imeitwa ala ya muziki. Ingawa ni watu wachache tu wanaoweza kuimba kama mwimbaji wa opera, kwa watu wengi, kuimba ni jambo la kawaida kama vile kula ama kulala. Iwe unaweza au huwezi kuimba vizuri, bila shaka utapendezwa kuchunguza jinsi “ala” hiyo inavyofanya kazi.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgtKuVOCYRmBS35CVHwSEC9XKw_zvlFt9zFXK3bf9eFqfByWGt-aheUjzibmOE63GDP9y7UWhaOeeLdn4EdWe-p9aLj0a2__B1AAycCP8UaVHMd9hUz0NsQDgkrTLp-UHCj4UWTtnaKLNg/s1600/Shusho2.pngChristina Shusho (Tanzania)

Zoloto ambayo iko katikati ya koo, ndicho hasa kiungo kinachotokeza sauti. Imefanyizwa kwa gegedu inayozunguka shimo lenye misuli miwili, yaani, nyuzi za sauti. Sauti hutokezwaje? Kwa kawaida mtu anapopumua, nyuzi hizo hulegea na kufanyiza mwanya wenye umbo la pembetatu katika koromeo. Unapoimba, hewa husukumwa kwa nguvu kupitia zoloto, mwanya huo huwa mwembamba, nazo nyuzi za sauti hutikisika na hivyo kutokeza sauti. Kadiri nyuzi hizo zinavyokazika ndivyo zinavyotikisika zaidi na kutokeza sauti nyembamba zaidi. Kwa upande mwingine, kupunguza shinikizo la hewa kunalegeza nyuzi za sauti, kunafanya mwanya huo uwe mpana, na hivyo kufanya nyuzi za sauti zisitikisike sana na kutokeza sauti nzito zaidi.

Ustadi na Umbo la Mtu
Akiwa kijana, Enrico Caruso alikuwa na sauti nzuri sana lakini haikuwa na nguvu. Mazoezi yalisaidia kufanya sauti yake iwe yenye nguvu. Sauti tamu ni kipawa cha asili, lakini ustadi ni muhimu katika muziki wa opera. Mwimbaji anapaswa kujua jinsi ya kupumua ili awe na hewa ya kutosha. Kisha anapaswa kujifunza jinsi ya kuidhibiti hewa hiyo. Inasemekana kwamba Carlo Broschi, mwimbaji maarufu wa karne ya 18, anayejulikana kama Farinelli, angeweza kudhibiti hewa sana hivi kwamba angeweza kuimba noti 150 za muziki bila kuvuta pumzi.

Pia, waimbaji wa opera wanahitaji kujifunza kukuza sauti wakitumia mwili wao. Kulingana na wataalamu fulani, mifupa ya kifua ndiyo inayotumiwa kukuza sauti nzito huku taya na mifupa ya uso ikitumiwa kukuza sauti nyembamba zaidi.

Wengi wanafikiri kwamba kuimba kunahusisha tu kutumia koo. Hata hivyo, imegunduliwa kwamba mwili wote unahusika, yaani, mtu hutumia nguvu zake zote kuimba. Usawaziko mzuri unahitajiwa ili misuli katika sehemu zote za mwili ifanye kazi kwa upatano. Hivyo, kuimba opera kunahitaji jitihada na nguvu nyingi, na huenda hiyo ndiyo sababu waimbaji fulani wa opera ni wanene na wenye nguvu. Maria Callas alikuwa mmoja wa waimbaji maarufu zaidi wa opera katika karne ya 20, lakini wengi wanaamini kwamba sauti yake ilidhoofika kwa sababu ya kupunguza uzito haraka kwa kubadili chakula alichokula.

Mabadiliko Katika Uimbaji wa Opera
Kadiri ambavyo wakati umepita, mtindo na mbinu za kuimba opera zimebadilika. Acheni tuzungumzie mifano miwili tu. Opera ilipoacha kuimbwa katika makanisa na majengo madogo na kuanza kuimbwa katika majumba ya opera, waimbaji walianza kutumia miili yao kama vikuza sauti badala ya kuimba kwa sauti nyororo, kwa mtiririko bila jitihada nyingi. Mabadiliko hayo yalizidishwa wakati okestra ndogo kama ile ya Mozart zilipoacha kutumiwa na badala yake kukawa na okestra kubwa zaidi kama ile ya Verdi na ya Wagner. Katika karne ya 17 na ya 18 na pia sehemu ya karne ya 19, uimbaji wa opera ulitegemea kabisa uwezo na ustadi wa mwimbaji. Mtindo uliotumiwa katika nusu ya pili ya karne ya 19 na sehemu ya kwanza ya karne ya 20 ulikuwa tofauti kabisa. Katika kipindi hicho, sauti ijapokuwa muhimu, ikawa mojawapo tu ya vitu muhimu katika uimbaji wa opera.

Uwezekano mkubwa wa opera kuwa maarufu ulichochea kutokeza muziki kwa wingi. Watungaji kama vile Paisiello, Cimarosa, Gluck, Mozart, Donizetti, Rossini, Bellini, Wagner, Verdi, Puccini, Bizet, Meyerbeer, na Mascagni, ambao walikuwa baadhi ya watungaji mashuhuri sana, walitunga baadhi ya nyimbo zisizosahaulika na zinazoweza kuchochea hisia za ndani.

Kupita Mipaka Katika Uimbaji wa Opera
Pia, kumekuwa na mambo yasiyopendeza katika historia ya opera. Wafikirie wakastrati, ambao kwa zaidi ya karne moja walikuwa sehemu muhimu ya opera ya Italia.* Wavulana walihasiwa kabla ya kubalehe ili wadumishe sauti zao nyembamba sana zinazoweza kusikika mbali na zenye nguvu sana. Guido Tartoni anasema kwamba zoea hilo lilitokea kwa sababu “kanisa, . . . lilikataa wanawake . . . wasiimbe kanisani.”

Waimbaji maarufu wa opera wamekuwa mashuhuri sana, na baadhi ya wapenzi wa muziki wao wamewaabudu. Mfano mmoja wa ibada hiyo ulionekana wakati wa mazishi ya Luciano Pavarotti yaliyofanyika. Maria Callas aliitwa La Divina (Mungu), na Joan Sutherland, La Stupenda (wa Ajabu). Hata hivyo, umaarufu wowote wa opera umetokana na uwezo wake wa kuwasisimua wasikilizaji.

Huenda wakati ujao ukasikia sauti ya wimbo mtamu sana. Hilo likitukia, tua na ufikirie mazoezi na jitihada zilizohitajiwa ili kutokeza sauti hiyo tamu. Huenda hilo likakuchochea uanze kuuona uimbaji wa opera kama mwandishi mmoja aliyeuita njia ya “kuunganisha maneno na muziki na kuyapa mashairi . . . mabawa ya muziki.”

SOMA ZAIDI BONYEZA HAPA

Comments