PETE YA NDOA KWENYE NDOTO INAWEZA KABISA KUWA AGANO NA MASHETANI. KARIBU TUJIFUNZE NDOTO NA MAANA ZAKE.
BWANA YESU asifiwe!
Leo Natoa Tahadhari Za Ndoto Na Nakuletea Baadhi Ya Ndoto.
Chunga Sana Unapoota Ndoto Unavalishwa Pete Au Unafunga Ndoa, Ukiota Hivyo Muombe Sana MUNGU. Maana Ndoto Za Namna Hiyo Zina Maana Nyingi, Unaweza Ukaota Unafunga Ndoa Na Mtu Iwe Unamfahamu Au Humfahamu Lakini Maana Yake Ikawa Unafunga Ndoa Na Majini, Na Kama Uliota Ndoto Za Namna Hiyo Usishangae Kuishi Miaka 60 Bila Kuolewa Au Kuoa Kama Hukujua Jinsi Ya Kumwita BWANA YESU Ili Akusaidie, Maana Huyo Jini Uliyefunga Nae Ndoa Ndotoni Atawakimbiza Wanadamu Wote Wanaotaka Kukuoa Labda Tu Wawe Na YESU Na Wajue Jinsi Ya Kuvunja Nguvu Za Giza.
Maana Ya Pili Unaweza Kuota Unavalishwa Pete Na Kijana Yeyote Yule, Na Kwasababu Unataka Tu Kuolewa Ukafurahi Sana Kumbe Maana Yake Ulikua Unaingia Maagano Na Mashetani. Na Maagano Hayo Ili Yafutike Unatakiwa Uokoke Na Uombe Au Uombewe Maombi Ya Kuvunja Maagano Yote Ya Tangu Utotoni.
Maana Ya Tatu Inaweza Kuwa Unafunga Ndoa Na Kazi Yako Na Uchunge Kazi Yako Isije Ikakukosesha Mbingu,
Na Maana Ya 4 Inaweza Kuwa Ni Kweli yaani umeona tukio sahihi kwamba utafunga ndoa.
Ngoja Nikupe Siri Hii;
Adui Zako Hutafuta Kukumaliza Katika Ulimwengu Wa Roho Wala Sio Ulimwengu Wa Mwili, Ulimwengu Wa Roho Ndio Ule Uuonao Katika Ndoto, Lakini Watu Wengi Hudharau Ndoto Wanazoota. Endapo Wewe Ni Tajiri Katika Ulimwengu Wa Roho, Hivyo Hivyo Katika Ulimwengu Wa Mwili Utakuwa Tajiri. Na Kama Unateseka Sana Kwenye Ndoto Usishangae Sana Maana Hata Kwenye Ulimwengu Wa Mwili Utateseka Kama Usipojua Ufanyeje.
Ndugu Yangu Nakuomba Usidharau Ndoto Unayoota, Bali Kila Ndoto Husika Nayo. Kama MUNGU Amekuonyesha Wachawi Wakikuwinda Wala Usiseme Kwamba "hii Ni Ndoto Ya Shetani" Mshukuru MUNGU Kwa Kukuonyesha Na Anza Kuomba Ukiwapiga Kwa Moto Wa Damu Ya YESU, Hao Maadui Uliowaona Ndotoni, Kama Ndoto Ni Ya MUNGU Akikuonya Basi Kubali Kuonyeka, Kama Ni shetani Anakulaghai Mponde Kwa Nyundo Maana Neno La MUNGU Ni Nyundo.
Tuache Ka Tabia Haka Kwamba Ukiona Ndoto Ya Mambo Ambayo Huyapendi Unasema Hiyo Ndoto Ya shetani Na Ukiota Ndoto Ya Kuendesha Gari Unasema Ni Ndoto Ya MUNGU Kumbe Hata Adui Hulaghai.
Naendelea Na Tahadhari Za Ndoto. Uwe Makini Sana Unapoota Unakula Chakula Ndotoni, Tena Omba Sana Ukiota Unatafuna Na Kumeza Chakula Ndotoni. Mara Nyingi Mapepo Au Mizimu Hayaingii Tu Kwa Mtu Hadi Watangulize Kwanza Vitu Vyao Na Hayo Hayo Wewe Utaota Unakula Kumbe Unameza Vitu Vya Kichawi.
Wachawi Nao Hukurushia Vitu Ambavyo Vitawafanya Wakuone Muda Wowote, Wewe Utadhani Umeota Ndoto Nzuri Ya Maakuli Kumbe shetani Yuko Kazini.
Kuna Dada Mmoja Aliota Bibi Yake Anamlisha Kipande Cha Nyama. Kesho Yake Akaenda Kanisani, Tulipomuombea Akatapika Nyama Ile Ile Aliyoiota Jana Yake.
Ndugu Usidharau Ndoto Unayoota Bali Mwite YESU Akuokoe Na Mitego Ya shetani Na Kumbuka Kwamba Moja Wapo Ya Dalili Za Kuwa Na Mapepo Ni Kuota Unatafuna Mizizi Au Chakula Na Mtu Anayesumbuliwa Na Mapepo Ukimuuliza Ndoto Ambazo Huziota Mara Kwa Mara Atakuambia Mara Kwa Mara Huota Anatafuna Vyakula. MUNGU Anakuwa Anakuonyesha Mipango Ya shetani Juu Yako, Usidharau Bali Omba Maombi Ya Vita Au Kimbilia Kwenye Maombezi. YESU Anakupenda Sana.
Kwenye Ndoto Ukiota Uko Ndani Ya Shimo, Ni Mbaya Maana Yake Uko Kwenye Kifungo Cha Adui, Jifungue Kutoka Kwenye Vifungo Ukitumia Mathayo 18:18, Wafilipi 2:10-11, Yohana 14:14, Mathayo 11:28 Na Marko 9:23.
Lakini Ukiota Mwanga Unamulika Katika Shimo La Giza, Ni Ndoto Nzuri Maana Yake MUNGU Ameingilia Kati Suala Lako, Mshukuru MUNGU Na Endelea Na Maombi, Tumia Mika 1:3 Na Isaya 54:17. Lakini Pia Ukiota Unatembea Nje Ya Shimo Au Bonde, Ni Vizuri, Inaonyesha Kuwa, Una Nguvu Za Kiroho. Mshukuru MUNGU Na Ongeza Maombi, Tumia Isaya 43:2-4. Lakini Pia Ukiota Kuna Ngazi Ya Kutokea Shimoni, Ni Ndoto Nzuri Maana Yake MUNGU Anafanya Kazi Kwa Ajili Yako. Endelea Na Maombi Kupitia Jina La YESU Kama Unavyofanya, Tumia Pia Zaburi 34. Lakini Pia Ukiota Unatembea Kutoka Kwenye Shimo La Giza Au Bonde La Giza Harafu Kuna Mtu Ambaye Anakurudisha Nyuma, Ni Mbaya, Maana Yake Kuna Maadaui Wanakurudisha Nyuma Kimaisha, Pigana Kiroho Kwa Kutumia Yeremia 1:10 Na Yeremia 1:19. Ubarikiwe Sana Na BWANA YESU Anakupenda Sana.
MUNGU akubariki sana na napenda kukushauri kuwa unaomba maombi ya vita pale ndoto uliyoiota unaijua kabisa kwamba umeonyesha na MUNGU kuhusu mipango mibaya ambayo shetani anakupangia katika ulimwengu wa Roho. Tumia maandiko haya katika kuomba Zaburi 68:20, Mithali 18:10, Yohana 14:14, Mathayo 11:28, Yeremia 1:10, Ufunuo 12:11, Luka 1:37, Marko 9:23 Na Yakobo 4:7.
Kwa sasa naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine.na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani. MUNGU ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA.
MUNGU akubariki sana .
Ni mimi ndugu yako
Peter M Mabula
Maisha ya Ushindi Ministry.
0714252292
mabula1986@gmail.com
MUNGU akubariki sana uliyesoma somo hili.
MUNGU Akubariki.
Comments