RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

HARUSI YA MWINJILISTI OCTAVIAN MAHEMBE NA CHRISTINA KIWHELE SIKU YA JUMAPILI 21.09.2014 YAFANA

Siku ya Jumapili 21.09.2014 Mwinjilisti wa kanisa la Yesu Kristo Huduma ya Maombezi na Uponyaji Mbezi Salsalasa la Mtumishi wa Mungu Nabii Flora, Bwana Octavian Mahembe aliweza kuonyesha msimamo wake kwa kuweza kufunga ndoa na Bi. Christina E Kiwhele. Ndoa hii ilifungishwa na mtumishi wa Mungu Nabii Flora Peter wa kanisa hilo.

Wanandoa hao walimshukuru sana Mungu kwa kuwawezesha kufikia yale malengo waliyoyapanga tangia wamechumbiana, pia walimshukuru sana Nabii Flora kwa malezi yake tangia walipojiunga na kanisa hilo na leo wamefunga ndoa, shukrani za kipekee walizitoa kwa wazazi wao waliowatunza mpaka kufikia umri wa kufunga ndoa na kuanza maisha mapya. Wanandoa hawa waliwashukuru wanakamati, waumini wa kanisa hilo, waimbaji, wageni waliofika kutoka mikoa mbalimbali, watu wa media, MC, ndugu na jamaa wote waliofika na wengine walioshindwa kufika kutokana na sababu zisizozuirika.

Hakika siku hii ilikuwa ya furaha sana katika ukumbi wa Motel Skyline uliko Mbezi Makonde hapa jijini Dar es Salaam Tanzania.

Zoezi la maandalizi ya harusi lilianzia kanisani kwa Nabii Flora baadae wanandoa wakiongozana na ndugu na jamaa walielekea Giraffe Hotel kwaajili ya picha na baadae kumalikia katika ukumbi wa Motel Skyline uliopo Makonde Mbezi.

kwa issue ya urembo, Bi Harusi alifanyia katika Saloon ya Jojo iliyoko Sinza Mapambano na Bwana Harusi alifanyia katika Barbashop ya B2.

Still picture na Video zimefanywa na Rumafrica +255 715 851523 www.rumaafrica.blogspot.com, Music na MC ni Obedi Kikao...



Mungu awabariki sana.







 Wazazi wa Christina Kiwhele

 Bwana Octavian akimfungua kitambaa Bi. Christina Kiwhwle
 Octavina na Christina Mahembe wakielekea madhabahuni
 Nabii Flora Peter akitoa sema jambo juu ya Bwana harusi na Bibi harusi
 Nabii Flora (kushoto) na Mchungaji Jury wakihubiri
















Comments