RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

NABII FLORA PETER AKIMUOMBEA NABII T.B JOSHUA KUHUSIANA NA GHOROFA YAKE KUPOROMOKA SCOAN

Nabii Flora ambaye ni mmoja ya watumishi wa Mungu wanaokubali sana huduma ya Nabii TB Joshua wa kanisa la SCOAN Nigeria, Jumapili ya tarehe 14.09.2014 aliweza kufanya maombezi na waumini wa kanisa lake la Yesu Kristo la Huduma ya Maombezi na Uponyaji lililoko Mbezi Mbuyuni Dar es Salaam.

Akiongea kwa masikitiko makubwa, Nabii Flora aliweza kukemea kazi za shetani zinazoharibu huduma ya Mungu na kuwavunja moyo watumishi wa Mungu, alisema yeye na jeshi lake la mbinguni wamejipanga kisawasawa kumuangamiza huyu shetani kwa kutumia jina la Yesu Kristo. Aliwaomba watu wote kumuombea Nabii TB Joshua na kanisa lake lote kwa msiba mkubwa waliopata na kuliombea Taifa la Nigeria. Aliwapa pole wafiwa na wale wote waliojeruhiwa na kupoteza mali zao katika ajali hiyo mbaya.
Nabii Flora Peter



Comments