RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

EXCLUSIVE: ELIZABETH NGAIZA ASHANGAZWA KUONA ATOSHA KISAVA NA MUME WAKE AMBWENE MWASONGWE WAKIMBILIA KWA MGANGA KUTAKA UTAJIRI

Ninatambua utakuwa unajiuliza ilikuwaje Atosha Kisava na mume wake Ambwene Mwasongwe kukimbilia kwa mganga kupata utajiri baada ya kuona maisha yao kuwa magumu sana wakiwa na mtoto mmoja ambaye baba yake sio Ambwene bali ni kutoka kwa mume mwingine.

Atosha Kisava baada ya kuolewa na Ambwene Mwasongwe akiwa na mtoto mmoja ambaye alizaa na mume mwingine, walimpenda sana mpaka watu wakawa wanatamani upendo walikuwa nao katika maisha yao. Wapendao hawa waliishi maisha magumu sana mpaka ikafika kipindi Atosha Kisava akaamua kufanya kazi ya kuuza pombe bar ili mradi tu apate chochote na maisha yaendelee mbele. Akiwa katika kazi yake ya kuuza pombe, Atosha Kisava akapata jaribu lingine la kukosa wateja, na hii ilimfanya awe na mawazo mengi sana yaliyosumbua moyo wake. Chakula kwao ilikuwa ni shida sana, kulala kwao ni kwa shida sana, kila kitu kilikuwa ni shida.

Elizabeth Ngaiza ashangazwa kuona Atosha Kisana na mume wake Ambwene Mwasongwe wakiwa katika maisha magumu.

Kitu alichoamua kukifanya Atosha Kisava baada ya kuona hapati wateja aliweza kwenda kwa mganga ili apate unafuu wa maisha. Mganga wa kienyeji aliweza kumpa masharti magumu sana Atosha Kisava kwa kumuomba alete mbuzi mmoja ili mambo yake yaende sawa. Atosha bila ya kujua lengo la mganga kumuomba huyo mbuzi lilikuwa ni nini..,  aliamua kumleta huyo mbuzi kwaajili ya sadaka ili tu maisha yake yaende sawa.

Watu husema ng'ombe wa masikini hazai, na hii ilimtokea Atosha Kisava kwani baada ya kupeleka huyo mbuzi kwa mganga bila ya kujua kwanini huyo mganga alimhitaji mbuzi na sio kitu kingine. Mganga huyo alimhitaji mbuzi akiwa na lengo la kumharibu mwanae na Atosha Kisava kuwa zezeta bila ya hata ya kumuambia Atosha. Hilo ndilo lilikuwa sharti kubwa la mganga la kuweza kumsaidia Atosha kuwa tajiri.

Mtoto wake na Atosha aliweza kuharibiwa akili yake na kuwa zezeta. Hali ya kimaisha ya Atosha Kisava ikiaanza kubadilika na kuwa na mafanikio makubwa sana, akiwa katika kazi yake ya bar, wateja waliweza kuongezeka sana na kumsababishia kupata fedha nyingi sana, na baadae aliweza kufanikiwa sana yeye na mume wake Ambwene Mwasongwe.

Siku moja waliweza kukaa chini na kutafakari maisha yao ya nyuma ambayo yalikuwa ya shida sana, jinsi gani walipata utajiri, je huo utajiri waliokuwa nao una faida yoyote mbele za Mungu na mbele za wanadamu, vipi kuhusu mtoto wao ambaye ni zezeta baada ya kwenda kwa mganga. Hayo yalikuwa ni baadhi tu ya vitu ambavyo walikuwa wakijiuliza. Mungu aliweza kuzungumza nao kwa njia anayojua YEYE, siku moja wakaamua kumgeukia Mungu na kufanya toba ya vile walivyofanya huko nyuma vya kumchukiza Mungu. Waliomba kibali kwa Mungu ili aweze kufuta dhambi zao na wabadilike ili wawe kondoo wake walio safi. Mungu alisikia kilio chao na kuwabadilisha na kuwa watumishi wa Mungu.

Maisha ya kumtumikia Mungu yakawa ni ya tofauti sana ukifananisha na huko nyuma, mawawzo yakawa ni kumtafakari Mungu na kufanya wawezalo kwaajili ya UTUKUFU wa Mungu. Mungu aliweza kuwabariki sana, na hakika wakafurahia wokovu wao. Na sasa ni watumishi wa Mungu wanaomsifu Mungu kwa njia ya uimbaji.

Sasa ndungu masomaji wangu, utakuwa unajiuliza maswali mengi kuhusiana na hii stori. Moja ya swali utakalotaka kujua ni Je, huyo mtoto zezeta ilikuwaje mwisho wake, Je, huyo mganga alipatwa na nini baada ya kuona wafuasi wake wamemsaliti na kumfuta Mungu? Majirani zake na ndugu zake wanawachukuliaje wanandoa hawa waliomuudhi Mungu kipindi cha nyuma?

Sasa ukitaka kujua mengi kuhusiana na hii stori basi nenda katika maduka ya kuuza DVD na CD na uliza Albamu ya ELIZABETH NGAIZA ya NASEMA NAO. Katika albamu hii yutapata mengi na ambayo hayajazungumziwa hapa.

Hii ni stori iliyotungwa na kuimbwa na mwimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania ELIZABETH NGAIZA katika albamu yake mpya ya NASEMA NAO, na wimbo uliobeba hiyo stori unaitwa AMELAANIWA. Albamu hii iko katika mfumo wa DVD na imetengezwa na studio ya HF iliyoko Tabata Chang'ombe hapa jijini Dar es Salaam Tanzania. Albamu hii ina nyimbo 8 na baadhi ya nyimbo ni Amelaaniwa, Wanene alakuwa (Kihaya), Siku ya Msiba wangu.

Maeneo yaliyofanyiwa hii DVD ni kama ifuatavyo: Bar iko Mwembeyanga Temeke, Nyumbani ni maeneo ya Shule ya Msingi Dovya, Kanisa lililotumika ni kanisa lilloko Sabasaba nyuma ya kanisa la PTA Sabasaba Temeke. Wahusika waliocheza waimbaji wa nyimbo za Injili ambao ni  Atosha Kisava, Ambwene Mwasongwe na Billman

Sasa unaweza kujipatia DVD hii ya SEMA NAO ya Elizabeth Ngaiza kwa kwa kumpigia simu +255 714 294 076 au Barua Pepe: elizabethngaiza@gmail.com.

Wahusika waliocheza clip hii Atosha Kisava na Ambwene Mwasongwe sio kweli kwamba ni mume na mke ila wameigiza tu, hawa ni watumishi wa Mungu safi wanaokubalika na jamii ya Kitanzania na kuheshimiwa kwa kazi zao nzuri za kumtumikia Mungu. Pia vitu vilivyozungumziwa sio kweli kwamba wao ndio waliofanya, ila walikuwa wakiwakilisha ujumbe kwako na mimi. Ila unatakiwa kujua hii stori ambayo ilishawahi kutokea na hawa wamefanya kuwakilisha ili ujifunze.

|MUNGU WANGU NA AKUBARIKI SANA

 Kutoka kushoto ni Crew ya HF, Elizabeth Ngaiza, Atosha Kisava na cameraman wakiwa katika maandalizi.
 Atosha Kisava (kushoto) akipata maelekezo kutoka kwa camera man.
 Atosha Kisava full shangwe.
 Kulia ni Elizabeth Ngaiza mwenye hii DVD ya NASEMA NAO akiwa ametoka counter kuweka mambo sawa tayari kwa shooting.


Atosha Kisava akiwa bar akiuza pombe..
 Ambwene Mwasongwe akiwa nyumbani kwake, wakiishi maisha ya taabu sana na mke wake Atosha Kisava.
 Oooh Jamani leo mchana tutakula nini na mke wangu Atosha Kisava..?? Haya ni maneno ya Ambwene Mwasongwe akitafakari kwa makini.
 Atosha Kisava akitoa nguo zake kwaajili ya kuzifua na mume wake mpendwa Ambwene Mwasongwe.
 Atosha Kisava: Mume wangu usilie vumilia tu haya ni mapito, tutashinda tu mume wangu..nakupendwa mwaya....
 Ambwene Mwasongwe: Duh...!! Mke wangu Atosha, hapa mgongoni panauma, sijui kwaajili ya uchovu wa kazi za shamba...?
 Ambwene Mwasongwe: Mwanangu usihofu, hizi shida ni za muda mfupi tu, tutakuwa matajiri, sawa..?
 Atosha Kisava: Duh nguo zenyewe chafu mpaka basi..na sabuni yenyewe haitoshi, sijui nikaombe kwa jirani yangu Elizabeth Ngaiza..?
 Atosha Kisava: Mume wangu mpenzi Ambwene, usiweke sabuni nyingi, nguo zenyewe kama unavyoziona hazitoshei hii sabuni...
 Ambwene: Yaaah...sasa nguo iko sawa mke wangu, imetakata au unasemaje mwanangu?
 Atosha Kisava: Mume wangu ndio maana nakupenda, unajua kutumai vizuri sabubu na maji haya ya shida, nguo imetaka, sasa leo nitakufurahisha mume wangu...sawa?
 Ambwene Mwasongwe: Sasa sikilizeni..nimeona kama vile mambo yetu yanakwenda kuwa safi...!! Mke wangu utakuwa katika maisha mazuri na mwanangu utaenda shule nzuri..sawa?. Mtanikumbuka na mtakumbuka hapa tulipokaa
 Atosha Kisava na mume wake Ambwene Mwasongwe wakielekea kwa mganga ili afanya mambo maisha yao yabadilike.
 Ambwene Mwasongwe: Mke wangu huku tunakoenda kwa mganga ndiko yaliko majibu yetu..tunaenda kufanikiwa na chochote atakachosema mganga tutatimiza..au unasemaje mke wangu?
 Atosha Kisava: Mume wangu Ambwene njoo taratibu hapa kuna mteremko mkali sana, anagali usije ukaanguka...njoo nikushike mkono.
 Atosha Kisava: Yaani mume wangu Ambwene, nimechoka na maisha haya ya kushinda bar bila wateja na hali yetu ni ngumu sana..ngoja huyu mganga afanye kweli..au unasemaje mume wangu?
 Ambwene Mwasongwe: Kweli mke wangu Atosha..mimi ninakuamini kwa kila jambo, hata akitupa sharti gani tutatimiza..Mke wangu una akili sana..ila tu huna akili ya kimafanikio na ndio maana tunateseka..nakutania mke wangu...usinune
 Ambwene Mwasongwe: Yaani leo maji ni kidogo sana, toka tumeondoka kwenda kwa mganga mpaka sasa, maji yamekuwa chini sana...sijui itakuwaje huko nyumbani na hatukuacha hata maji ya kupikia..!!
 Ambwene Mwasongwe: Ngoja nifunge huu mfuniko tuondoke, labda tukija baadae maji yatakuwa yameongezeka.
 Nadhani nimefunga sawasawa...

BAADA YA KUTOKA KWA MGANGA ATOSHA NA MUME WAKE AMBWENE MAISHA YAKO YAMENYOOKA NA SASA WANAMILIKI GARI
 Kutoka kulia ni Elizabeth Ngaiza (mwenye hii DVD ya NASEMA NAO, Atosha Kisava na Ambwene Mwasongwe
 Ambwene Mwasongwe: Sasa maisha safi sana, mke wangu ana akilisana...
 Ambwene Mwasongwe: Ngoja nimfuate mke wangu na tuelekee kanisani..tuachane na maisha ya kumtumikia shetani.

ATOSHA KISAVA NA AMBWENE MWASONGWE SASA WAMEAMUA KUMTUMIKIA MUNGU NA KUOKOKA.
 Kulia ni Elizabeti Ngaiza na Atosha Kisava wakiwa madhabahuni
Ambwene Mwasongwe akiwa madhabahuni akifanya kazi ya Bwana baada ya kuokoka.

Mpiga Picha: Hizi picha lazima nikazirushe mtandaoni leoleo ni make story.
Hii ni gari ya Ambwene Mwasongwe..sio utani ni ukweli kabisa watumishi wa Mungu. Ameinuliwa bado wewe kuinuliwa. Piga magoti na utii kile Mungu anasema kwa kupitia Neno lake na watumishi wake waliopo hapa duniani.

Mwandishi:
Rulea Sanga
Rumafrica For Alll Nations
www.rumaafrica.blogspot.comwww.rumaafrica.blogspot.com
+255 715 851 523

Comments