RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

FRIEND OF JESUS (FOJ) WAMZAWADIA TV MZEE DANIEL LYANGA KWA KUWA MWALIMU WA SUNDAY SCHOOL KWA MIAKA 50

Friend Of Jesus (F.O.J) ni kikundi cha wanaharakati wa mambo ya Yesu katika kanisa la KKKT Kariakoo jijini Dar es Salaam. Kikundi hiki ambacho kimejipatia wajumbe wengi sana wenye moyo wa kumpenda Yesu Kristo kwa kupitia mtandao wa watsap. Mpaka sasa kikundi kimefanya mambo makubwa sana kuokoa mioyo ya watu na pia kusaidiana wakati wa shida na raha. FOJ kwa sasa imewanganisha wajumbe wake kutoka katika kanisa hilo la KKKT Kariakoo, na kinampango wa kuwa na wajumbe kutoka nje ya kanisa hilo.

Siku ya Jumapili ya 12.10.2014 FOJ iliungana na waumini wa kanisa hilo kumpongeza na kumzawadia Mzee Daniel Lyanga kwa kuwa mwalimu wa Sunday School katika kanisa hilo kwa muda wa miaka 50. Mwalimu Daniel amewafundisha wachngaji mbalimbali na sasa wana majina makubwa sana, kama vile Mch. Lewizi Hiza wa Kanisa la KKKT Chuo Kikuu Dar es Salaam, Mch. Mzonga wa kanisa la KKKT Azania Front dar es Salaam na wengine wengi.

FOJ ilitoa zawadi ya TV kubwa ya LG kama pongeza kwa kazi ya Mungu anayofanya na aliyofanya kipindi cha nyuma. Siku hiyo ilikuwa ni sku ya shangwe na ndelemo kanisani hapo, na jina la Bwana lilitukuzwa.

Mungu azidi kumlinda Mwalimu Daniel Lyanga na azidi kuibarika kazi ya mikono yake ili izidi kusonga mbele na watu wamjue vizuri huyu bwana wetu Yesu Kristo.

Comments