RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

JUMAPILI HII 02.10.2014 VICTORARON KUZINDUA ALBAMU YAKE YA KANUNI 2x2

Wapenzi na washabikiwa mambo ya Mungu na mnaopenda kumsifu Mungu kwa kupitia nyimbo, Jumapili hii ndugu yenu na rafiki yenu Victor mwana wa Aron atakuwa akizindua albamu yake. Unaombwa sana kumuunga mkono kwa kufika eneo husika. Jumapili hii itakuwani siku ya kipekee sana kwa mwana wa Aroni kuikabidhi kazi yake kwa mwenyezi Mungu ili aweze kupata kibali machoni pa wanadamu na machoni pa Baba yetu wa Mbinguni. Itakuwa njema sana na wewe ukihusika na kushuhuda Mungu atakavyofanya siku hiyo.
Mwana wa Aron siku hiyo ataimba LIVE nyimbo zaidi ya tano kutoka katika albamu yake mpya na ile albamu ya kwanza ataimba ule wimbo unaoupenda na uliyomtangaza Victor Aron katika ulimwengu wa muziki wa Injili. Siku hiyo tegemea jambo la neema kufanyanyika katika maisha yako, itakuwa ni siku ya baraka juu ya baraka.

Kutakuwa na waimbaji mbali mbali ambao utawaona siku hiyo wakimsindikiza ndugu yetu Victor Aron. Mungu wetu hupenda sana kuona watu wanatumia muda wao kumsifu na kumshukuru wakiwa wamekusanyika pamoja.






MUNGU AKUTIE NGUVU UFIKE SIKU HIYO

Comments