RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

MH. FREDRICK SUMAYE KUWA MGENI RASMI KATIKA UZINDUZI WA DVD YA 2 x 2 YA VICTOR ARON JUMAPILI HII

Waziri Mkuu Mstaafu Mh. Fredrick Sumaye atakuwa mgeni rasmi katika tamasha hili kubwa la mtumishi wa Mungu Victor mwana wa Aron katika kanisa la DCT Tabata Shule Dar es Salaam. Tuna kila sababu ya kumshukuru Mh. Fredrick Sumaye kwa kutenga muda wake kwajili ya kushiriki tamasha hili la kuzindua albamu ya Victor Aron inayoenda kwa jina la Kanuni au 2x2. Tunatambua kuwa ana majukumu mengi kwaajili ya ujenzi wa Taifa letu, lakini ameweza kukubali kuungana na kijana wake. Mungu azidi kumpigania Mh. Fredrick Sumaye kwa kazi zake na mipango yake aliyoipanga.

Mh. Fredrick Sumaye

Tamasha hili litaambatana na uimbaji kutoka kwa waimbaji mbalimbali kama vile Christina Shusho, Madam Ruti, Christopher na wengine wengi. Uzinduzi utafanyika siku ya Jumapili 02/11/2014 kuanzia saa 8 mchana, kwahiyo unaombwa kuwahi mapema ili ujipatie nafasi nzuri ya kukaa. Mbali na uzinduzi tamasha hili limeandaliwa kwaajili yako wewe kuja kumsifu Mungu, na hakuna kiingilio kabisa.

Victor Aron

Victor Aron ataimba LIVE nyimbo zaidi ya tano kwa utukufu wa Mungu.Akiongea na Rumafrica, alisema yeye na crew yake wamejiandaa vya kutosha na hawana wasiwasi kabisa siku hiyo, kwahiyo anaomba sana watu wafike na ikiwezeka kila mmoja aje na marafiki zake kupokea baraka zao kwa njia ya sifa.

ANGALI TANGAZO UTAJIFUNZA JAMBO


Tangazo limetengezwa na Rumafrica +255 715 851 523

Comments