RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

RULEA SANGA AMEPATA PIGO KUBWA TENA NA KUONDOKEWA NA RAFIKI YAKE MAREHEMU ALPHONCE MATEMBO KWA AJALI YA PIKPIKI

Nimepokea taarifa za kifo cha rafiki yangu Alphonce Matembo kwa masikitiko makubwa sana siku ya tarehe 13.10.2014 pale tu nilipokuwa naelekea ofisini kwangu Afrikasana Sinza. Nilikutana na Mzee Rajabu ambaye alikuwa karibu na ofisi yangu na akaanza kuniambia kuwa yule rafiki yetu Alphonce Matembo amefariki dunia kwa ajali ya pikipiki. Ajali hiyo ilitokana na mwendesha pikipiki kumfuata marehemu na kumgonga nyuma na pale pale marehemu alifariki dunia pamoja na dada mmoja aliyekuwa nyuma ya hiyo pikipiki. Tunamshukuru Mungu kwa kila jambo, kwani dereva alipona hata kama amepata majeraha.

Rulea Sanga kwenye gari upande wa kulia akielekea makaburini kumzika rafiki yake Alphonce Matembo.

Nakumbuka kabla ya kifo chake marehemu siku nne nyuma tuliweza kukaa naye na kuongelea masuala ya kazi na tukapanga yafanyike siku ya Jumapili baada ya mimi kutoka ibadani, marehemu alinikubali na aliniahidi kufanya kwa uaminifu. Wakati naongea naye alionekana ni mtu wa furaha sana, na kumbuka marehemu alikuwa ni mtu wa kupenda kuongea sana na kuchekesha hasa unapofika wakati wa majibizano ya michezo. Alphonce Matembo alikuwa na tabia ya kusoma magazeti ya michezo na hasa gazeti la Mwananchi, kila nilipokuwa nikimuona asubuhi na mapema wakati anelekea ofisini, nilimuona akiwa na gazeti la michezo.

Marehemu Aliphonce Matembo alipenda sana kunitania na kuniita "Sanga". Marehemu amenifanyia vitu vingi sana na kitu ambacho aliweza kuniachia ni pale tu alipoweza kupaka rangi ya ofisi yangu na nyumbani kwangu ninakoishi. Huu ni ukumbusho wangu kwake. Alphone ni mtu aliyekubalika sana na jamii inayonizunguka hapa Afrikasana. Inaumiza sana kuona leo hii siko naye tena.

Kabla ya kifo chake, siku hiyo ya tarehe 13.10.2014 alipigiwa simu na mpenzi wake Morogoro siku yake ya kuzaliwa, akiongea kwa utani na ucheshi mbele ya marafiki zake waliokuwepo mahali pale kama mzee Rajabu, Mhina, Maasai, na wengine waliokuwepo, aliweza kuongea kwa ucheshi na furaha kwa mpenzi wake na kumuahidi kumtumia zawadi ya kuzaliwa kwake. Tunaweza kusema, Alphonce Mutembo amefariki siku ambayo mpenzi wake ni siku ya kuzaliwa kwake.

Nakumbuka nilipomuona kwa mara ya kwanza siku hiyo ya kifo chake alikuwa amevalia singilendi yake nyeupe huku akiongea na simu yake. Baada ya muda kama nusu saa hivi, aliweza kuvaa shart lake huku akiwa amebeba kibegi chake cha vifaa vya kazi akielekea eneo la kazi. Huko ndiko aliweza kupata ajali ya pikipiki. Inaumiza sana

Marehemu amepumzishwa katika nyumba yake ya milele maeneo ya Kiluvia Dar es Salaam, akiwa ameacha watoto wake wawili akiwa na umri wa miaka 38, na ni mwenyeji wa mkoa wa Songea.
 Maiti ikiingizwa katika nyumba ya Baba yake maeneo ya Kiluvia


KIPINDI CHA KUAGA MWILI WA MAREHEMU ALPHONCE MUTEMBO






 Rulea akionekana kwa mbali akiwa na ndugu na jamaa wakiupeleka mwili wa marehemu kwenye gari.


 Kulia ni rafiki yake na marehemu Alphonce ambaye alikuwa wa kwanza kupokea simu na kutaarifiwa kifo cha Alphonce
 Aneonekana nyuma akiwa ameshikiliwa ni mdogo wake na marehemu Alphonce
 Rulea Sanga (kulia kwenye gari akielekea makaburini)

MWILI WA MAREHEMU ALPHONCE MUTEMBO UKISUBIRIWA KUWEKWA KWENYE NYUMBA YAKE YA MILELE MAENEO YA KILUVIA

 Anayepiga picha ni rafiki yake wa karibu sana wa marehemu Alphonce ambaye alikuwa akifanya naye katika ofisi moja Afrikasana Sinza anaitwa MHINA
 Mhina (aliyevalia shati la blue) akihakikisha rafiki yake na mfanyakazi mwenzake marehemu Alphonce akizikwa.
 Kulia ni rafiki wa marehemu Alphonce, mzee Rajabu akifuatiwa na Mgoni, hawa ndio waliokuwa wkipishana na kuhusiana na jinsi gani ya mtu kumkumbuka mpenzi wake siku ya kuzaliwa kwake, baada ya mabishano kilichofuata ni kifo cha marehemu.

Comments