RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

SHUHUDA MOTOMOTO KUTOKA KATIKA KANISA LA YESU KRISTO HUDUMA YA MAOMBEZI NA UPONYAJI MBEZI SALASALA DSM KWA NABII FLORA PETER


NENO LA MUNGU LINATOKA KATIKA KITABU CHA ZABURI 103:1-8
Biblia inasema:  Ee nafsi yangu umuhimidi Bwana, naam, vyote vilivyo ndani yangu vilihimidi jina lako takatifu, ee nafsi yangu umuhimidi Bwana wala usizisahau fadhili zake zote. Akusamehe maovu yako yote, na akuponye magonjwa yako yote; usisahau matende makuu Mungu aliyokutendea, usisahau pale Bwana alipokutana na wewe akabadilisha maisha yako, usisahau kule Mungu alikokutoa. Nataka mchana wa leo watu wasamehewe maovu yao yote, ndipo Bwana awaponye magonjwa yao yote, ukiona mtu ameshuhudia amepona  Bwana amemsamehe maovu yake yote, na kisha amemponya magonjwa yake yote.
Biblia inasema;  Aukomboa uhai wako na kaburi, akutia taji ya fadhili na rehema, aushibisha mema uzee wako, ujana wako utarejezwa kama tai Bwana ndiye afanyae mambo ya haki, na hukumu kwa wote wanaoonewa ; yaani uzee wako utashibishwa mema, utaonekana kijana kila siku, Mungu arudishe miaka yako na sura yako. huu ni mwezi wa kibali na ni wiki ya maombi, Bwana aurejesha ujana wako kama tai.

SOMA SHUHUDA HIZI ZITAKJENGA

SALOME KINABO ANAMSHUKURU MUNGU BAADA YA KUTUMIA STICKER AMEPATA HAMU YA KULA NA PIA AMELIPWA DENI ALILKUWA ANADAI

Bwana Yesu asifiwe, naitwa Salome kinabo; namshukuru Mungu, nilikuwa na tatizo la kukosa hamu ya kula, nilikuwa nakula mlo mmoja kwa siku. Lakini baada ya kutumia sticker ya Nabii Flora sasa hivi naweza kula milo mitatu, pia namshukuru Mungu kuna mtu nilikuwa namdai deni langu sasaivi amenilipa.
BABA ANAMSHUKURU MUNGU MAISHA YAKE YAMEKUWA MAZURI BAADA YA KUOMBEWA NA NABII FLORA
Bwana Yesu asifiwe; nilikuja kwa Nabii Flora nikiwa na hali mbaya sana ya kiuchumi, nilikuwa sipati pesa kabisa, namshukuru Mungu toka nimekuja kwa Nabii Flora sasa hivi hali yangu ni nzuri sana, maisha yangu yamekuwa mazuri na yametulia.
DADA ANAMSHUKURU MUNGU ALIKUWA AMEISHIWA NGUVU NA TUMBO KUJAA LAKINI BAADA YA KUTUMIA STICKER NA MAJI YALIYOOMBEWA NA NABII FLORA AMEPONA

Bwana Yesu asifiwe; namshukuru Mungu sana sticker ya Nabii Flora na maji yamenitendea mambo makubwa, nilipulizia dawa ya mbu kazini hapo hapo niliishiwa na nguvu nikaanza kubanwa na tumbo lilijaa. Lakini kupitia mtumishi wa Mungu aliniombea vitu vilitembea tumboni na Mungu aliteenda miujiza. Nilifika kazini nikaanza kumwaga maji ya Nabii Flora na kusema damu ya Yesu itembee, na Mungu ametenda, namshukuru sana Mungu.
DADA ANAMSHUKURU MUNGU BAADA YA KUTUMIA SABUNI ILIYOOMBEWA NA NABII FLORA MTOTO WAKE AMEPONA KIDONDA NA YEYE PIA KICHEFUCHEFU KIMEMWISHA

Bwana Yesu asifiwe; namshukuru Mungu wa Nabii Flora sabuni imenisaidia, mtoto wangu alikuwa na kidonda hakiponi, lakini baada ya kutumia sabuni iliyoombewa na Nabii Flora kwa muda wa siku mbili mtoto wangu akapona. Na mimi nilikuwa nasikia kichefuchefu kama mtu mjamzito, nilichukuwa sabuni nikaiweka tumboni namshukuru Mungu imenisaidia.

NEEMA ANAMSHUKURU MUNGU MWANAYE AMETEMBEA BAADA YA KUTUMIA STICKER YA NABII FLORA   Bwana Yesu asifiwe, naitwa Neema; namshukuru Mungu wa Nabii Flora amenitendea mambo makubwa, mwanangu alikuwa atembei, lakini baada ya kutumia sticker ya Nabii Flora sasa hivi anatembea, namshukuru sana Mungu.  

ELIBARIKI  MAGERE ANAMSHUKURU MUNGU KWA KUPATA KAZI BAADA YA MAOMBI YA NABII FLORA

Bwana Yesu asifiwe, naitwa Elibariki Magere ni Mwinjilisti; toka nimefika kwa Nabii Flora nilikuwa sina kitu nilikuwa sina kazi, lakini leo Mungu ameniinua nimepata kazi.

Niliiyacha familia yangu Mwanza kwa muda wa miezi nane, lakini sasa Mungu amenipa kibali nimepata nyumba maeneo ya Salasala, na hivi nategemea kuondoka siku ya Alhamisi kwenda Mwanza kuichukuwa familia yangu, namshukuru Mungu sana, napenda kuwaambia kwamba Mungu wa Nabii Flora anaonekana, na pia msipende kutangatanga kwa maana ukisoma Zaburi ya 1:3 inasema kwamba naye atakuwa kama mti uliopandwa kando kando ya vijito vya maji.

ELIZABETH CHARLES ANAMSHUKURU MUNGU BAADA YA KUTUMIA STICKER YA NABII FLORA NA MAJI MUWASHO UMEKWISHA

Bwana Yesu asifiwe, naitwa Elizabeth Charles natokea Shinyanga; Namshukuru Mungu wa Nabii Flora amenifanyia mambo mengi sana. Nilikuwa nawashwa makwapa nikivaa nguo, alafu cha ajabu shetani alivyo na nguvu nilikuwa nikikutana na watu ndio nazidi kuwashwa. Nilinunua sticker nikampelekea Nabii nikamwomba aiombee, Nabii akaikunja ile sticker akaiweka kwenye maji, nilipofika nyumbani nikaogea yale maji na nikanywa kwa imani. Nilipoamka asubuhi nikavaa nguo nikajiona nipo vizuri na muwasho hakuna tena, namshukuru sana Mungu.

 FLORENCE ANAMSHUKURU MUNGU BAADA YA KUTUMIA STICKER NA SABUNI ILIYOOMBEWA NA NABII FLORA AMEKUBALIKA KWA NDUGU NA PIA AMEPATA KIBALI CHA KWENDA KUFANYA INTERVIE 
          
Bwana Yesu asifiwe,  naitwa Florence, natokea Kimara mwisho
; namshukuru Mungu amenitendea mengi kwa sababu nilikuwa na roho ya kukataliwa, ndugu zangu wamenikubali kuanzia sasa hivi. Na pia nilikuwa kila sehemu nikienda kuomba kazi nakataliwa siitwi hata kwenye interview, hivi ninavyoongea kuanzia saa kupitia sticker na sabuni iliyoombewa na Nabii Flora, kesho tarehe 20 nimeitwa kufanya interview, namshukuru sana Mungu

ELIZABETH SILVESTER ANAMSHUKURU MUNGU AMEFUNGA NDOA KAMA NABII FLORA ALIVYOMTABIRA, NA PIA AMEFUNGULIWA KATIKA MAPEPO ALIYOTUMIWA NA MAMA YAKE MKUBWA
Bwana Yesu asifiwe, naitwa Elizabeth Sylvester;  namshukuru Mungu mwaka jana Nabii alinitabiria nitafunga ndoa mwezi huu wa kumi, na kweli imetimia kwangu. Na baada ya kufunga ndoa mama yangu mkubwa alinitumia mapepo ili niachike kwa mume wangu, lakini namshukuru Mungu wa Nabii Flora amenifungua

ELIZABETH GABRIEL ANAMSHUKURU MUNGU KWA KUMPONYA MATATIZO YA TUMBO PAMOJA NA VIDONDA VYA TUMBO BAADA YA KUTUMIA STICKER NA SABUNI
Bwana Yesu asifiwe, naitwa Elizabeth Gabriel; nilikuwa nasumbuliwa na tumbo mara kwa mara pamoja na U.T.I, namshukuru Mungu baada ya kuja kwa Nabii Flora na kuombewa sasa hivi nimepona, na nyumbani kwetu familia yetu imekuwa na furaha na vicheko vimetawala. Na pia nilikuwa nasumbuliwa na vidonda vya tumbo, lakini baada ya kutumia sticker na sabuni sasa hivi nimepona, namshukuru sana mungu.

JEN MWAMFILIJA ANAMSHUKURU MUNGU KWA KUSAFIRI SALAMA NA KUREKEBISHA NYUMBA YAKE SALAMA BAADA YA KUTUMIA STICKER YA NABII FLORA NA PIA NYUMBA YAKE IMEPATA MPANGAJI      
Bwana Yesu asifiwe,  Jen Mwamfilija;  nilikuja katika madhabahu ya Nabii Flora nilikuwa nasafiri naenda Mbeya, nilikuja kwa Nabii Flora kuomba kibali cha kusafiri,na pia nyumba yangu ilikuwa inamatatizo wapangaji hawakai na pia ina mambo ya kishirikina, nilimwambia vyote Nabii Flora. Nikamwomba Nabii ninunue sticker ili kwenda kuzifukia katika nyumba yangu, Nabii alisema sawa na akaziombea, akaniombea na kwaajili ya safari nilikuwa nasafiri na gari yangu. Namshukuru Mungu nilifika salama na zile sticker nikafanya kama nilivyomwambia Nabii, niliondoka na mafundi kwa sababu nilikuwa naenda kurekebisha nyumba yangu. Mafundi walitumia sticker kwa kunywa na kunawa, waliweza kutoa mabati yako kwa sababu nyumba ilikuwa inavuja. Siku ya pili yake ilinyesha mvua kubwa sana dari yote ikalowana, nilimpigia Nabii simu lakini ilipokelewa na watumishi wengine wakaniambia niendelee kuwa na imani.  Namshukuru Mungu mafundi walimaliza salama japo kwenye paa walikutana na mijusi ya ajabu, na pia siku ambayo naondoka nyumba yangu ilikuwa haipati wapangaji lakini siku hiyo nikapata mtu akachukuwa nyumba na nikalipwa kodi ya mwaka mzima.   

JULIUS ANAMSHUKURU MUNGU KWA KUSAMEHEWA DENI BANK BAADA YA MAOMBI YA NABII FLORA


Bwana Yesu asifiwe, naitwa Julius; nilinunua sticker ya Nabii Flora nikakaanayo mfukoni, nilikuwa na deni bank la milioni kumi na tisa, nikawa nawalipa kila mwezi laki moja. Baada ya miezi mitatu wakaja wakaniambia lipa milioni nne alafu tukusamehe deni lililobaki, nikasema hapana hiyo pesa ni nyingi sana, baadaye tena wakaja wamaniambia nilipe milioni mbili na laki saba alafu iliyobaki wananisamehe, nikawaambia sawa, namshukuru sana Mungu.
 
LUCY SHABANI ANAMSHUKURU MUNGU KWA KUPATA MCHUMBA BAADA YA KUTUMIA STICKER YA NABII FLORA  
                                                                   
Bwana Yesu asifiwe, naitwa Lucy Shabani
; Namshukuru  Mungu wa Nabii Flora amenitendea kupitia sticker, hii sticker nilienda kuioge, baada ya muda nikakutana na mtu ambaye simfahamu, nilikuwa natoka kupokea mahari ya mtoto wa ndugu yangu. Alipita kaka mmoja kituoni na tulikuwa watu wengi, Yule kaka akaniambia dada naomba nikuchukuwe nikupeleke maana na mimi naelekea huko unakokwenda, mimi nikasema hapana, Yule kaka alinilazimisha sana, basi nikakubali tukaondoka, kufika njiani nikamwambia mimi nishushe hapa akasema hapana nitakupeleka mpaka unapokaa. Wakatu tunaingia njia ya kuingia kwangu gari ikaingia kwenye mchanga ikazama, akawa anampigia mke wake simu akawa hapokea, akanielekeza nyumbani kwake nikamwambie mke wake aje na gari nyingine ili amvute, nilienda kumwambia wakati narudi nikakuta kuna watu wamefika pele wameizingira ile gari, walikuwa wametoka Kanisani, wale watu wakasema sisi tumetoka Kanisani tuna nguvu ya Mungu hii gari tunaivuta wenyewe, kweli wakaivuta ikatoka, na mimi nikaondoka zangu. Baada ya wiki mbili nikakutana na Yule kaka akiwa amevimba jicho, nikamwambia kaka unanikumbuka, akasema hapana, nikamkumbusha kuwa kuna siku usiku alinipa lifti, akakumbuka lakini amepatwa na matatizo mke wake amefariki, na jicho alilovimba ni shemeji yake alimpiga ngumi wakati akiwa anayaombea maji, yeye ameokoka ila mke wake ni mwislamu. Aliniomba namba yangu ya simu nikampatia, baada ya akaniambia nilikuwa nataka mke aliyeokoka sasa nimeona wewe ndeye, na nilikuwa nataka mwwanamke mwenye umri mkubwa. Namshukuru Mungu nimepata mchumba na mwezi wa kumi na mbili tunafunga ndoa, hii ni baada ya kutumia sticker ya Nabii Flora.

KAROLIN MARTIN ANAMSHUKURU MUNGU MWANAYE MARY KUPONA KATIKA HALI MBAYA ALIYOKUWA NAYO BAADA YA KUOMBEWA NA NABII FLORA
Bwana Yesu asifiwe, naitwa Karolin Martin; nina binti yangu anaitwa Mary, juzi siku ya Alhamisi alisema kwamba amesikia harufu ya damu, Ijumaa asubuhi nikamwambia aje kwa Nabii Flora, Nabii akamwombea. Alivyofika nyumbani hali ilibadilika sana, tukamleta tena kwa Nabii Flora akiwa amezia kabisa hata alikuwa ahemi , kwa kweli Mungu wa Nabii Flora anatisha sana, nilikuwa namshikia na kuona kwa watu lakini nimemshuhudia mimi mwenyewe kwenye familia yangu. Nabii alimwombea na mpaka sasa hivi binti yangu ni mzima kichwa hakiumi tena na mauti imefutwa kabisa.
Mary akielezea jinsi ilivyomtokea; ilikuwa ni siku ya Alhamisi nilianza kusikia harufu ya damu chumbani kwangu, nilitoka chumbani nikaenda sebuleni bado hali ikawa ile ile, nilitoka nikaenda migombani
ambako niliona nitajiskia vizuri lakini niliendelea kujiskia vibaya. Ilipofika mchana nikaanza kusikia kichwa kinauma sana, nikilala kinatulia lakini nikiamka nasikia kinauma kama kimepigwa shoti, Alhamisi sikulala kabisa usingizi usiku kucha, nilikuwa naumwa na kichwa naota ndoto za ajabu ajabu, mara naota watu wananikimbiza, mara mwingine ameshika panga, lakini huyo aliyekuwa ameshika panga alivyokuwa ananikimbiza nikaanguka chini. Lakini huku na huku kulikuwa na wamama wawili mmoja ananiita huku na mwingine huku, lakini kuangalia vizuri mmoja alikuwa ni mama yangu mzazi, basi nikawa namwambia mama mimi siwezi kuamka hapa nilipo. Ijumaa asubuhi nikampigia mama simu nikamwambia nasikia sana harufu ya damu, mama akaniambia niende kwa Nabii Flora, nilitoka nilipofika mbuyuni nilikoswa koswa na gari, watu wakaniambia wewe dada unawaza nini unaona sasa unataka kusababisha matatizo. Nikaondoka nikaenda nyumba, nilipofika kituo cha kuvukia nyumbani nilisimama muda mrefu sana bila kuvuka barabara, kila nikitaka kuvuma roho ilikuwa inakataa, nikasubiri mpaka magari ya huku na huku hamna kabisa ndio nikavuka. Nilipofika nyumbani mdogo wangu akaniambia dada umekula nikamwambia mimi sijiskii kula, yeye akaenda kuchukuwa chakula akala, mimi nikaingia ndani nikalala nikawa nimevua nguo, mdogo wangu akaja akaanza kunicheka akasema dada umeona bora ulale bila nguo, akaniambia basi vaa nguo. Nikatoka nikaenda sebuleni tumbo wazi nimevaa tu suruali nikawa nasikia moto, nikaanza kutapika sana, mdogo wangu aliogopa akaenda akamwita jirani akasema ngoja niazime pesa nikupeleke hospitali maana simu ya mama napiga haipokelewi. Nakumbuka nilipomaliza kutapika nikainuka, nilipoinuka nikaona kitu kimenipitia kama shoti, hapo ndio nilidondoka kutoka hapo nikawa sijui chochote ndio nikaletwa kwa Naabii Flora, nilishtuka saa nne usiku ndio nikaanza kutambua watu.


GETRUDI MWANGOSHI ANAMSHUKURU MUNGU KWA KUPONA FANGASI BAADA YA KUTUMIA  STICKER ILIYOOMBEWA NA NABII FLORA
 Bwaana Yesu asifiwe, naitwa Getrudi Mwangoshi; namshukuru Mungu, kupitia ile sabuni tuliyopewa jumapili, Nabii alisema watu wenye fangasi wapite mbele waombewe. Nilikuwa na fangasi ambazo haziponi, namshukuru Mungu nilivyoenda kuogea sabuni siku ya kwanza, ya pili, ya tatu zikakauka, namrudishia Mungu sifa na shukrani.
MAMA ANASHUKURU MUNGU KWA KUPATA BEGI LAKE LILILOKUWA LIMEIBWA
Bwana Yesu asifiwe; nilikuwa nafanya usafi hapa Kanisani, kuna mtu akaniibia begi langu, namshukuru Mungu begi langu limerudishwa na kila kitu.

MAMA KIDAMI ANAMSHUKURU MUNGU MUME WAKE AMEPONA MKANDA WA JESHI BAADA YA KUPAKWA MAFUTA NA KUOMBEWA NA NABII FLORA
Bwana Yesu asifiwe, naitwa mama Kidami; Namshukuru Mungu wa Nabii Flora amenitendea, mume wangu alianza kutokwa na viupele usoni, nikachukuwa sabuni iliyoombewa na Nabii Flora nikamwambia nawia. Kwenye maji yake ya kuoga nikawa namwekea sticker, lakini vipele vikaendelea kutoka upande mziwa wa uso na kichwa, akaenda hospitali akaandikiwa sindano tano, alichomwa sindano tatu hali haikubadilika ndio inazidi. Mwanagu Musa akamwambia baba hii siyo hali ya kawaida twende kwenye maombi, baba akakataa, nilichukuwa sabuni ya Nabii Flora nikaomba nikasema, ee  Mungu wa Nabii Flora kama unatendea watu na wanafanikiwa naomba unipe kibali cha kuitikiwa na mume wangu kwenda Kanisani. Alikuwa amekaa nje kwa sababu ndani anaungua joto, nilimwambia mume wangu tuingie ndani kuna kitu nataka nikwambie, akaniambia haya, tukaingia ndani tukakaa, nikwambia mume wangu hii dalili uliyonayo sio ya kawaida, na hii dalili inaonyesha kama vile unamkanda wa jeshi, nikamwambia naomba mume wangu twende Kanisani, sikulazimishi kubadilisha dini lakini nakuomba twende Kanisani, akaniambia basi nimekubali. Tuliondoka naye tukaja mpaka Kanisani, tulimuona Nabii Flora, Nabii alichukuwa mafuta akampakaa ile sehemu ambayo imeungua inamapele mengi. namshukuru Mungu alimtendea tulipofika nyumbani hakupandisha joto na vile vipele vyote vilikauka, ilipofka asubuhi vipele vilikauka vyote na kulala alilala, nikamwambia mume wangu umeamini kweli yupo Mungu anayeponya, akasema kweli nimeamini.  

MAMA MCHAKI ANAMSHUKURU MUNGU MWANAYE BAADA YA KUTUMIA STICKER YA NABII FLORA AKAJIFUNGUA SALAMA NA YEYE BAADA YA KUOGEA SABUNI ILIYOOMBEWA NA NABII FLORA MWANAYE AMEMPIGIA SIMU                                                            
Bwana Yesu asifiwe, naitwa mama Mchak
i; Namshukuru Mungu amenitendea kupitia sticker ya Nabii Flora, mtoto wangu alishidwa kujifungua, aliambiwa atajifungua kwa operation. Lakini baada ya kuchukuwa sticker ya Nabii Flora akajigusisha tumbo, namshukuru Mungu alijifungua kawaida. Na pia kuhusu sabuni iliyoombewa na Nabii Flora, mtoto wangu alikuwa hajanipia simu kwa muda mrefu sana, lakini baada ya kutumia sabubni ya Nabii Flora nilipoiogea na kuigandisha katika mwili wangu, jana yake Nabii alisema watu wote watapigiwa simu, na kweli siku hiyo hiyo usiku nikapigiwa simu, namshukuru Mungu wa Nabii Flora.

MAX ANAMSHUKURU MUNGU WA NABII FLORA KWA KUMPONYA VIPELE BAADA YA KUTUMIA STICKER YA NABII FLORA   
Bwana Yesu asifiwe, naitwa Max Msangwa kutoka Mwanza
; namshukuru Mungu wa Nabii Flora kwa sababu amenitendea makuu, nilikuwa na viupele vingi sana mwilini. Nilitumia sticker ya Nabii Flora na siku moja Nabii aliniambia nitapona, namshukuru Mungu nilipoamka asubuhi vipele vikawa vimekauka vyote, namshukuru sana Mungu wa Nabii Flora.

RICHARD MPANGALA ANAMSHUKURU MUNGU MAMA YAKE AMEPONA BAADA YA KUTUMIA STICKER YA NABII FLORA   
Yesu asifiwe, naitwa Richard Mpangala natokea Njombe, kwa hapa Dar es salaam nakaa Bahari Beachi
; kupitia sticker ya Nabii Flora nilipoenda Njombe mama yangu aliweza kupona, namshukuru sana Mungu.

THERESIA ANAMSHUKURU MUNGU AMEPATA MCHUMBA NA MAMA YAKE AMEPONA KUPOOZA NA PIA YEYE AMEPAJA AJIRA BAADA YA KUOMBEWA NA NABII FLORA
wana Yesu asifiwe, naitwa Theresia; namshukuru sana Mungu wa Nabii Flora kwa sababu amenitendea mambo mengi katika maisha yangu. Mimi na familia yangu tulifika kwa Nabii Flora tukiwa tunaumwa, tumetekwa na mizimu ya nyumbani, tulikuwa hatuwezi kuolewa, siku moja nilikuja kwa Nabii akaniuliza unataka nini, nikamwambia nataka kulewa, Nabii akaniambia utaolewa mwanangu, na kweli imetokea mwaka huu nimepata mchumba na kweli nimekuwa Engaged , harusi yangu ni mwezi wa kumi na moja tarehe 29, namshukuru Mungu sana.

Pia mama yangu alikuwa anaumwa alipoona upande mzima, tulifika kwa Nabii Flora akiwa hawezi kutembea, lakini sasa hivi anaendelea vizuri na fimbo aliiacha Kanisani. Pia nilifanya kazi miaka mitatu kulipwa ilikuwa ni shida, nafanya kazi lakini nikikaribia kulipwa wanasema hatuoni kazi unayoifanya, nilimweleza Nabii, Nabii akaniambia nitalipwa kwa wakati, na nikamwambia nataka kuajiriwa nimechoka kufanya kazi Temporary, akasema basi utaajiriwa. Ilipita wiki moja nikaitwa kwenye interview, nimekaa nyumbani nikapigiwa simu nimefaulu, na sasa hivi nimeajiriwa na ninapata haki zangu zote, namshukuru sana Mungu.

Comments