RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BAADHI YA WAIMBAJI WATAKAOVAMIA JUKWAA KATIKA UZINDUZI WA DVD YA AMETENDA YA VENERANDA BUGERAHA NA KUONYESHA MAVAZI YA MKRISTO KUVALIWA (FASHION SHOW) SIKU YA KESHO JUMAPILI

Ilikuwa miezi na sasa ni masaa, yumesubiri sanaaa,,na sasa wakati umefika wa watu wa Mungu kwenda katika sehemu zetu za kujidai na kufuraha na Mungu wetu tunayemwabudu kila siku. Sehemu kama hizi ni za makutano wa Wakristo kuweza kubadilisha mawazo, kujifunza na kupata elimu kutoka kwa waimbaji wetu wa nyimbo za Injili,

Sasa Jumapili hii ya tarehe 30.11.2012 Wakristo wote na watu wote jijini Dar es Salaam na kutoka katika mikoa mbalimbali tutakuwepo katika ukumbi wa kisasa kabisa wa LANDMARK HOTEL ulioko Ubungo Riverside barabarani kabisa. Katika eneo hilo tutashuhudia live kumuona dada yetu mpendwa VENERANDA BUGERAHA akizindua albamu yake mpya ya AMETENDA katika mfumo wa video.

Veneranda Bugeraha
Mbali na uzinduzi kutakuwa na waimbaji wa nyimbo za Injili watakaoonyesha mavazi ya kuvaliwa kwa mkristo katika maeneo mbalimbali ambayo yatamtambulisha huyu kuwa ni mucha Mungu na mwenye hofu ya Mungu, mwenye kujiheshimu na kufuata maadili ya Mtanzania. Kwahiyo siku hiyo kufana sana, na haijawahi kutokea kuona waimbaji wa nyimbo za Injili wanajiingiza katika maswala ya ubunifu wa mavazi na pia kufanya fashion show.

Tamasha hili litaanza saa 7:00 mchana na kuendelea, kiingilio kwa watoto ni 2,000/- na wakubwa ni 5,000/ tu. Tunakukaribisha sana na kumbuka kuja na mwenzako akupe kampani siku hiyo...
 Joshua Mlelwa
 Stella Joel
Furaha Isaya
 Atosha Kissava
 Beatrice Mwaipaja
 Madam Ruti
Upendo Nkone
 Silas Mbise
 Grace Rwegasha
Mess Jacob Chengula
 Manesa Sanga
 Ibrahim Sanga (kulia)
Smart Boy

Comments