RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

CHAMA CHA MUZIKI WA INJILI TANZANIA KIKIFANYA MAOMBEZI NYUMBANI KWA MH. MARTHA MLATA KIJIJINI KWAKE USHORA KIBAYA - SINGIDA

Mwandishi na mpiga picha: Rumafrica
Chama cha Muziki wa Injili Tanzania (CHAMUITA) kikiongozwa na mlezi wa chama hicho Mbunge wa Viti maalumu (CCM) mkoani Singida Mh. Martha Mlata kiliweza kufika katika kijiji cha Ushora Kibaya wilaya ya Iramba kwa lengo la kufanya umisheni, kuhubiri Neno la Mungu, kupanda miti (utunzaji wa mazingira), kuliombea taifa la Tanzania, kufanya tamasha kubwa la waimbaji kutoka kwa waimbaji maarufu Tanzania na pia kuonyesha filamu za maisha ya Yesu Kristo kwa wakazi wa kijiji hicho.

Mh. Martha Mlata

Baada ya kuwasili katika kijiji hicho, waimbaji na wachungaji waliweza kufika nyumbani kwa Mh. Martha Mlata na kufanya maombezi kabla ya kuanza huduma ya umisheni. Mh. Martha Mlata alikuwa na machache ya kuzungumza kwa wageni waliomtembelea ikiwa ni pamoja na kuwashukuru kwa kufika eneo la kijiji chake kwa kazi ya Mungu.

Mh. Martha Mlata-Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Singida

Baada ya maombezi kufanyika Mh. Martha Mlata akiongea kwa unyeenyekevu kwa wageni waliomtembelea nyumbani kwake alikuwa na haya ya kusema;
"Bwana Yesu Asifiwe waimbaji na wachungaji, nina kila sababu ya kumshukuru Mungu kwa kutuwezesha kuona siku njema ya leo ambayo tunaianza kwa furaha kwa kumtukuza Mungu wetu. Tunawashukuru sana wageni waliofika kutoka Dar es Salaam kuungana na sisi ili kuweza kuanza tamasha letu la uimbaji pamoja na kumtukuza Mungu kwa kupitia mahubiri na maombi. Ninaamini Taifa letu linakwenda kuponywa, kwahiyo tunashukuru sana.

Mh. Martha Mlata akiongea na wachungaji na waimbaji

Hili ni tamasha la Neno la Mungu na mkutano ambao ninaamini utakuwa wa miujiza kwa siku hizi tatu. Lakini Baba Askofu nataka kukuambia kwamba, sisi hapa tumekuja na miti ya matunda kwasababu tunakumbuka Mungu alivyoumba ulimwengu, aliumba mwanadamu katika bustani nzuri sana yenye matunda, kwahiyo tunataka kuwahimiza Watanzania wote kupitia ujio wetu huu hapa, ni kwamba tuyatunze mazingira yetu ambayo mwenyezi Mungu alitupa kwa kupata hasa miti ya matunda, kwahiyo sisi kesho tutakuwa na kazi kubwa ya kupanda miti yetu ya matunda na kutunza mazingira kwa kupanda miembe. Baada ya miaka miwili tutaanza kula miembe. Ninawashukuru sana kwa kunisikiliza


Tuone baadhi ya picha za waimbaji na wachungani wakifanya maombezi.
 Waimbaji na wachungaji wakifanya maombi rasmi kwaajili ya umisheni
 Kutoka kulia ni Joyce Ombeni, Mch. Bupe Kingu, Lilian, Mch. Vaileth (Arusha), John Shabani, Jesca (aliyekaa), Mh. Martha Mlata, Jane Misso, Mwandishi wa habari, Askofu wa Singida, Edson Mwasabwite, Mchungaji kanisa la KKKT Ushora Kibaya, MC.





 Edson Mwasabwite (kulia)
 Mch. Vaileth kutoka Arusha (kulia) akifuatia John Shaban
 Mh. Martha Mlata akiwashukuru wachungaji na waimbaji kwa kufanya maombezi nyumbani kwake tayari kwa kazi ya Mungu.
 Mh. Martha Mlata (katikati)


 Cameraman Danny akihakikisha matukio yanarekodiwa
 






SAFARI YA KUELEKEA KATIKA VIWANJA VYA KKKT USHORA KIBAYA KWA HUDUMA YA UMISHENI

Baada ya maombezi kumalizika nyumbani kwa Mh. Martha Mlata, waimbaji wa nyimbo za Injili kwa mara ya kwanza walifunga safari kuelekea katika viwanja vya kanisa la KKKY Ushora Kibaya ambako shughuli nzima ya umisheni ilikuwa ikifayika.

Waimbaji hawa baada ya kuona watu wengi wamekuwa wakifanya huduma mijini tu na kusahau kuwa kuna watu vijijini hawapati mafundisho ya Mungu na hawatiwi moyo na waimbaji wakubwa ambao kwa neema ya Mungu wamekubalika na jamii na kuheshiwa, waliona sasa ni wakati wa kuhubiri injili vijijini.

Sasa ngoja tuone baadhi ya picha za waimbaji wakielekea katika viwanja vya kanisa la KKKT Ushora Kibaya.

Edson Mwasabwite (kulia) akiwa ameongozana na Mh. Martha Mlata

 Edson Mwasabwite na Mh. Martha Mlata wakiwa katika picha ya pamoja
Mh. Martha Mlata (kulia) na Ann Annie

Kutoka kulia ni Camera man Dany, Mh. Martha Mlata na Edson Mwasabwite
Kulia ni Rulea Sanga wa Rumafrica
Waimbaji na wachungaji wakielekea katika eneo la tukio kwa kazi ya Bwana


Jane Miso wa Omoyo

Lilian (kulia) akiwa na Mh. Martha Mlata
Mh. Martha Mlata akishuka
WAIMBAJI BAADA YA KUFIKA KATIKA VIWANJA VYA KANISA LA KKKT USHORA KIBAYA KWA HUDUMA YA UMISHENI

Ikiwa ni siku ya kwanza kwa waimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania kukanyaga katika viwanja vya kanisa la K.K.K.T Ushora Kibaya wilaya ya Iramba mkoa wa Singida, wanakijiji waliwapokea waimbaji hawa kwa nderemo na vifijo wakiongozwana Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mh. Martha Mlata. Waimbaji na wachungaji walioalikwa walionekana wenye kushangazwa na maandalizi waliyoyakuta katika viwanja hivyo ikiwa ni pamoja na jukwaa kubwa lenye viwango vya kimataifa likiwa limefungwa kijijini hapo.

Mh. Martha Mlata kwa mara ya kwanza wakicheza katika viwanja vya kanisa la K.K.K.T Ushora Kibaya.

Mh. Martha Mlata alionekana akiwa na furaha kubwa sana kuona waimbaji wenzake wameweza kukanyaga katika viwanja vya Ushora kwa kazi ya Mungu. Mh. Martha Mlata ni mmoja wa walezi wa Chama Cha Muziki wa Injili Tanzania na pia ni mwimbaji maarufu sana wa nyimbo za Injili, alweza kumshukuru sana Mungu kwa wema wake na kuwalinda waimbaji na wageni wote walioalikwa katika shughuli ya umisheni.

Mh. Martha Mlata wa tatu kutoka kulia

Lengo kubwa la waimbaji kufika katika kijiji hiki cha Ushora Kibaya ni kufanya umisheni, kufundisha Neno la Mungu, kuwaombea wenye uhitaji na kuwafungua waliofungwa na vifungo vya shetani, kupanda miti kama moja ya utunzaji mazingira, kuonyesha filamu za maisha ya Yesu  kwa wanakijiji hao, kuwaelimisha wanakijiji na kuwaburudisha kwa njia ya uimbaji.


Wa pili kutoka kushoto ni Katibu Mwenezi wa Chama Cha Muziki wa Injili Tanzania (CHAMUITA) Stella Joel akifuatia Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mh. Martha Mlata na ni Mlezi wa CHAMUITA,

Katika ziara hii kulikuwa na wachungaji, wainjilisti, walimu na viongozi mbalimbali wa dini walioweza kuhudhuria mkutano huu mkubwa.

Kwaya ya kanisa la KKKT Ushora Kibaya ikiwakaribisha wageni kwa nyimbo za nguvu.



Sasa ngoja tuone baadhi ya picha zinazoonyesha jinsi wanakijiji walivyowapokea wageni wao tarehe 14.11.2014.




 Mh. Martha Mlata (kushoto) na Stella Joel
 wa tatu kutoka kushoto ni mwimbaji Paffii
 Wa tatu kutoka kulia ni mwimbaji Ann Annie kutoka Arusha
Kutoka kulia ni MC kutoka Ushora, Jane Misso, Stella Joel, Mh. Martha Mlata, Askofu mkoa wa Singida



Gari lililokuwa limebeba generator kwaajili ya umeme.


BAADA YA KUFANYA UZINDUZI, WAIMBAJI WALIEKEA NYUMBANI KWA MARTHA MLATA KWA CHAKULA CHA MCHANA
Baada ya kumtumiakia Mungu waimbaji na wachungaji walirudi nyumbani kupata chakula cha mchana

Mch. Bupe Kingu (kushoto) na Mch. Vaileth (Arusha)
Katibu Mwenezi wa Chama cha Muziki wa Injili Tanzania, Stella Joel
Rulea Sanga (kulia) na Ann Annie
Rulea Sanga (kulia) na Ann Annie
Kutoka kulia ni Mh. Martha Mlata, Mh. Margreth Sitta








Comments