RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

"MUNGU AMENIHURUMIA ASILIAMIA 100" NDIO HABARI YA WAKRISTO SASA..EDSON MWASBWITE ANAIZINDUA ALBAM HII JUMAPILI


Ukifika Tanzania utakumbana na habari mpya ya "MUNGU AMENIHURUMIA ASILIMIA 100" kutoka kwa mwimbaji maarufu sana Tanzania na nje ya Tanzania, Edson Mwasabwite anayejulikana kwa kibao chaki kinachopendwa na wamana hasa na pia wababa cha "NI KWA NEEMA NA REHEMA"

Mungu amempa kibali kingine cha kutoa albamu yake ya pili ambayo anakwenda kuizindua Jumapili 07.12.2014 katika kanisa la K.K.K.T Sinza kumekucha kuanzia saa 7:00 mchana na kuendelea. Hakutakuwa na kiingilio chochote, ni wewe kuwa na nauli yako ya kuja na kuondokea baada ya tamasha. Unaombwa sana kuja na rafiki zako na ndugu zako siku hiyo na pia sambaza habari hizi kwa watu wengi kwa kuwatumia ujumbe kwa njia ya simu au kuwapigia simu, ili nao siku hiyo wasikose baraka za Mungu kutoka kwa mwimbaji Edson Mwasabwite.

Edson Mwasabwite

Edson Mwasabwite ambaye kwa bahati mbaya hana wazazi yaani yeye ni yatima, amekuwa akiomba sana mwenyezi Mungu amsaidia ili naye awe asali kwa yatima wenzake waopitia maisha magumu kama aliyopitia tangia akiwa mtoto. Kwahiyo wewe unayepitia maisha kama hayo na wewe uliyebahatika kuwa na wazazi unaombwa sana kuungana na Edson Mwasabwite siku hiyo kuwatia moyo yatima na wenye uhitaji.

Tamasha hili litakuwa na waimbaji wengi sana,  baadhi yao ni kama unavyowaona katika tangazo hapo chini.

Tangazo limetengezwa na Rumafrica +255 715 851 523

Comments