RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

"MUNGU ANAWEZA" NDIO HABARI MPYA DUNIANI KUTOKA KWA MWIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI TANZANIA TUMAINI NJOLE

Mwimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania ametoa albamu yake ya pili inayoenda kwa jina la MUNGU ANAWEZA baada ya kuwika na albamu yake ya kwanza ya SEMA NA YESU.
Katika  albamu hiyo kuna nyimbo nyingi kali na zenye mguso wa ajabu sana ukizisikiliza, lakini kuna wimbo unaoitwa , SI MAZINGAOMBWE ILA MUNGU ANATENDA, wimbo huu unawatia moyo watumishi wa Mungu wanasemwa vibaya kutokana na huduma zao za kitumishi, ni mzuri sana ukiusikiliza.
Tumaini Njole

Tumaini Njole ambaye ametokea kupendwa na watu wengi sana mjini na vijijini kutokana na uimbaji wake na pia anavyoweza kulimudu jukwaa kwa kucheza. Watu wengi sana wanabarikiwa sana na uimbaji wa Tumaini Njole mwenye asili ya Dodoma Tanzania, na amewahi kufanya kazi na Rose Muhando kama ndancer wake miaka ya nyuma.

Upande wa mbele wa cover la Audio CD ya Tumaini Njole ya Mungu anaweza

Huu ni wakati wako wa kuitafuta hii Audio CD madukani au unaweza kuwasiliana naye kwa simu zinazoonekana katika cover la Audio CD yake. Kwa kupitia uimbaji utaenda kubarikiwa na kupokea miujiza yako kama utazingatia na kufanyia kazi kile ambacho mtumishi wa Mungu tumaini Njole amekiimba.

Upande wa nyuma wa cover la Audio CD ya Tumaini Njole ya Mungu anaweza

Mwimbaji huyu ambaye amebahatika kushiriki matamasha mengi sana nchini Tanzania na nje ya Tanzania na kujizolea sifa nyingi sana kwa kazi yake ya uimbaji, na pia ni mwimbaji mwenyeupendo kwa watu na muda mwingi ukimuona ni mtu wa kufurahi na kucheka. Kuna kitu Mungu amepanda ndani ya moyo wa Tumaini Njole, na hii inamsababishia kufanya vizuri sana akiwa anamtumikia Mungu.


Sticer ya cover la Audio CD ya Tumaini Njole ya Mungu anaweza

Katika historia ya maisha yake ni mwimbaji ambaye amepitia majaribu mengi sana ambayo kwa binadamu wa kawaida sio rahisi kuvumilia, lakini alipompokea Yesu Kristo kuwa mwokozi wa maisha yake hakika matatizo yote yalikwisha na ndio maana amebaki kumtumikia Mungu wetu wa mbinguni kwa kusifu na kuabudu.
Cover la Audio CD ya Tumaini Njole ya Mungu anaweza.

Rumafrica inafanya jitihada kumtafuta mwimbaji huyu ili kupata machache kutoka kwake ambayo tunaamini yatakujenga kiimani na maisha yako kwa ujumla. Ni mwimbaji ambaye akisimilia historia ya maisha yake hakika utaamini kuwa Mungu humtoa mtu kutoa sifuri na kwenda kwenye namba za maana.

Rumafrica imeshiriki kutengeza cover la Audio CD hii ya Tumaini Njole. +255 715 85 15 23



Comments