RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

NIPE NGUVU NDIO WIMBO MPYA TISHIO TANZANIA WA FLORA MBASHA

Unajua unapopitia magumu na mateso unahitaji msaada wa Mungu, wanadamu hawana msaada mkubwa wa kukusaidia ila Mungu tu anaweza. Mara nyingi tunavyoumizwa na wanadamu tumekuwa tukimkimbilia Mungu wetu kama Baba yetu na mfariji wetu. Tunahitaji sana nguvu za Mungu katika mapito yetu tunayopitia kila siku. Mungu wetu amekuwa msaada mkubwa sana kwetu na ametusaidia mengi na ndio maana tupo hapa tulipo. Hatuna budi kumuacha huyu Mungu wetu katika maisjha yetu.


Flora Mbasha

Flora Mbasha ambaye hivi karibuni alikumbwa na majaribu mengi katika maisha yake na hasa upande wa ndoa yake. Kutokana na hayo yote, hajateteleka kumtumikia Mungu wake ambaye amemfikisha hapa alipo. Huduma yake ya uimbaji imefanyika baraka kwa walio wengi hasa Tanzania na nje ya Tanzania. Serikali ya Tanzania imetambua mchango wake katika Taifa hili na amekuwa akitumia sana na viongozi wakubwa wa serikali katika kuhamasisha jamii kuenenda katika maadili mazuri. Hakika dada Flora Mbasha ni mtumishi wa Mungu na anapaswa pongezi nyingi kwa mchango wake mkubwa katika jamii yetu inayotuzunguka. Watu wengi sana wameokoka kwa kupitia huduma yake ya uimbaji.
NIPE NGUVU NDIO WIMBO MPYA TISHIO TANZANIA WA FLORA MBASHA

Flora Mbasha mbali na hayo yote aliyofanya na majaribu aliyopitia lakini bado aanazidi kumtumikia Mungu, na hivi sasa ametoa albamu yake ya NIPE NGUVU. Hakika ukisikia wimbo huu utamjua Flora Mbasha ni nani katika tasnia ya muziki. Mungu amekuwa mwema kwake kwa kumpa maneno mazuri yenye faraja na kufundisha jamii kuwa Mungu ndio kila kitu na ndiye mfariji wetu tunapopitia magumu.

Video imetengenezwa na kampuni ya X-Treme Videoz na kurekodiwa katika studio za Flem Studio



LIVE PERFORMANCE YA WIMBO WA NIPE NGUVU WA FLORA MBASHA


Comments