RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

SAFARI YA MWISHO YA GEORGE YAKAMILIKA, AZIKWA NA MAELFU KIWIRA

Hatimaye safari ya mwisho ya George ‘Bonge’ Njabili wa Mtoni "Lulu” Choir imekamilika baada ya mwili wake kurudishwa udongoni kwenye makaburi ya Kibumbe, Kiwira Mkoani Mbeya jana, majira ya saa saba mchana - mara baada ya ibada ya maazishi iliyofanyika kwenye Kanisa la Moravian Kiwira.

Maelfu ya watu wa jiji la Mbeya wamejitokeza kwa wingi kuaga mwili wa George Njabili, idadi ambayo haikutarajiwa, na hapo ndipo ikafahamika kwamba George ni mtu wa watu, na alikuwa akikubalika. Kwa mujibu wa shuhuda wetu, takribani zaidi ya watu elfu 4 walikuwepo huku wachungaji kadhaa pia wakiuaga mwili, ikiwemo Mchungaji Abiudi Misholi na Mchungaji Andulile kutoka Dar es Salaam.

Marehemu George ameacha watoto wawili na mke mmoja, Bi Tumpe. GK imefanikiwa kupata picha chache za kilichojiri kutoka kwa rafiki wa karibu wa marehemu, Mwinjilisti Danstan Mtoi, na nasi tunakufikishia.



Kabla ya safari, hapa ikiwa ni kanisani Mtoni

Makaburini, Kibumbe, Kiwira, Mbeya

Ni maombi yetu kwamba wafiwa wote watiwe nguvu kwenye kipindi hiki kigumu, BWANA alitoa na BWANA ametwaa, jina la BWANA lihimidiwe

Source: Gospel Kitaa

Comments