RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

SIKU YA KWANZA YA CHAMA CHA MUZIKI KUANZA HUDUMA YA UMISHENI KATIKA KIJIJI CHA USHORA KIBAYA WILAYA YA IRAMBA MKOA WA SINGIDA

Chama Cha Muziki wa Injili kwa mara ya kwanza kiliweza kufika nyumbani kwa Mh. Martha Mlata kama mwenyeji wao katika kijiji cha Ushora Kibaya wilaya ia Iramba Mkoa wa Singida. Dhumini ya ziara hii ilikuwa ni kufanya umisheni katika kijiji hicho, kufundisha Neno la Mungu kwa wanakijiji, kupanda miti kama moja ya kampeni ya kutunza mazingira, kuliombea Taifa la Tanzania, kuwaombea wenye uhitaji, kuonyehsa filamu za maisha ya Yesu na filamu mbalimbali zinazohusu maisha ya Mkristo, kuwaburudisha kwa nyimbo kutoka kwa waimbaji wa chama cha Muziki wa Injili Tanzania.

Baadhi ya waimbaji walioweza kufika katika tamasha hilo ni Jane Miso, Lilian, Edson Mwasabwite, Enock Jonas, Joyce Ombeni, Pafii, Yeronimo Mwalo, Stella Joel, Mh. Martha Mlata, Ann Annie, Tumaini Njole John Shabani, Mch. Bupe Kingu, Kwaya kutoka katika kanisa la KKKT Ushora Kibaya, waimbaji kutoka Arusha,  na wengine wengi.

Baadhi ya wachungaji ni Mch. Bupe Kingu, Mch. Vaileth kutoka Arusha, Wainjilisti kutoka Arusha, Maaskofu na wachungaji kutoka Ushora Kibaya.

Kulikuwa na waandishi wa habari kutoka Star TV kama Sauda Mwilima na Rumafrica ikiongozanan na Rulea Sanga na Danny

Hapo chini ni baadhi ya picha za waimbaji na wachungaji wakipokelewa na Mh. Martha Mlata nyumbani kwake Ushora Kibaya siku ya pili baada ya waimbaji kuingia usiku.


Hii ni nyumba ya Mh. Martha Mlata iliyopo katika kijiji chake alichozaliwa cha Ushora Kibaya wilaya ya Iramba mkoani Singida

Gari ya Mh. Martha Mlata ikiwa tayari kwa kazi ya Mungu.

Katibu Mwenezi wa Chama cha Muziki wa Injili Tanzania akishuka kwenye busi nyumbani kwa Mh. Martha Mlata
 Katibu Mkuu wa Chama cha Muziki wa Injili Tanzania kanda ya Kaskazini - Ann Annie akishuka kwenye busi nyumbani kwa Mh. Martha Mlata
 Lilian (kushoto)
Mh. Martha Mlata (wa tatu kutoka kushoto) akiwakaribisha wageni waliomtembelea nyumbani kwake Ushora Kibaya Singida
 Kutoka kulia ni Joyce Ombeni, Mch. Bupe Kingu, Yronimo Mwalo, Tumaini Njole, Mh. Martha Mlata na camera man Dany
 Joyce Ombeni (kushoto) akisalimiana na Mh. Martha Mlata
 Jane Misso (kushoto) akikumbatiana na Mh. Martha Mlata baada ya kukanyaga ardhi ya Ushora Kibaya wilaya ya Iramba
 Mh. Martha Mlata (wa pili kutoka kulia) akimpokea Mch. Vaileth kutoka Arusha

Haya ni mazingira ya kijiji cha Ushora Kibaya

KIPINDI CHA KUPATA CHAI TAYARI KWA SAFARI YA KUELEKEA KATIKA ENEO LA TAMASHA (VIWANJA VYA KANISA LA K.K.K.T USHORA KIBAYA
Kulia ni Jane Misso akiwa na Mchungaji wa kanisa la KKKT Ushora Kibaya

Kushoto ni mmoja wa waandishi wa habari waliofika siku hii kwa kupata matukio
waimbaji wakiombea breakfast. Kutoka kulia ni Ann Annie, Tumaini Njole na mchungaji kutoka Ushora Kibaya


John Shabani akipata chai


Comments