RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

SOLOMON MUKUBWA KUSHIRIKI KATIKA TAMASHA LA STELLA JOEL JUMAPILI HII


http://i.ytimg.com/vi/Jz_iNhHwRwY/hqdefault.jpg
Solomon Mukubwa
Mwimbaji wa nyimbo za Injili kutoka nchini Kenya Solomon Mkubwa siku ya Jumapili atakuwepo katika tamasha la uzinduzi wa albamu ya HAKUNA MWANAMKE MBAYA ya dada Stella Joel katika kanisa la KKKT Mabibo hapa jijini Dar es Salaam. Tamasha hili litakuwepo na waimbaji wa wengi sana ambao ni zaidi 20 kuvamia steji moja wakitumia mic moja kwa utukufu wa Mungu.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhp4kbVLKpa42LhK2h8G8-3gVszRmb0TeS8Hs8mRqEP5FDwBo7t9bnUiAT2BpJGbThl5v7ImyPU1xeBB9Ibn1aZk3lz19L8QPwKUfyPVYWmIdXyMVJNglInRyT57bPVxxC48VKbFDcjVxA/s640/DSC_0135.jpg
Stella Joel wa HAKUNA MWANAMKE MBAYA akiwa na mume wake Yeronimo Mwalo

Stella Joel akiongea na Rumafrica alisema hakika amejipanga vizuri sana kwa kazi ya Mungu. Amekuwa akimuomba sana Mungu ili siku hiyo watu wakapokee haja ya mioyo yao kwa kupitia uimbaji. Watu wategemee kupokea neema ya Mungu siku hiyo kwani waimbaji wamejiandaa kuhakikisha kazi ya Mungu inasonga mbele.
Siku hyo kutakuwa na projector ambapo watu wataweza kuona DVD ya dada Stella na hasa wimbo HAKUNA MWANAMKE MBAYA ambao umewashirikisha waimbaji wengi sana akiwemo Rose Muhando, DP, Janet Mrema, Yelonimo Mwalo, Mh. Martha Mlatha akiwa katika harusi ya dada Stella na wengine wengi sana.

Kwahiyo usikose kabisa kufika.


Comments