RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

TUINUE MUZIKI WA INJILI KUKUZA MAADILI KATIKA JAMII: UDA



Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA), Bw John Samangu (kushoto) akikata utepe kuzindua rasmi albamu ya kwanza kutolewa na ya kwaya ya Kanisa la Kigango cha Mtakatifu Rita wa Kashia ijulikanayo kama ‘Msifuni Bwana’ jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Wanaoshuhudia ni mwenyekiti wa Kigango cha Mt. Rita Bw. Frederick Msumali(kushoto) na waumini wengine.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA), Bw. John Samangu, akionyesha moja ya DVD wakati wa uzinduzi wa albamu ya kwaya ya Kigango cha kanisa la Mtakatifu Rita wa Kashia iitwayo ‘Msifuni Bwana’ jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Wanaoshuhudia ni Padre Xavery Kassase, Paroko Msaidizi wa Parokia ya Kanisa Katoliki la Mavurunza (kulia) na Mwenyekiti wa Kigango cha Mt. Rita Bw. Frederick Msumali(kushoto).

Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA), Bw John Samangu (kulia), akifungua moja ya kanda za albamu ya ‘Msifuni Bwana’ ya kwaya ya Kanisa la Kigango cha Mtakatifu Rita wa Kashia jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Anayeshuhudia ni mwenyekiti wa Kigango cha Mt. Rita Bw. Frederick Msumali (kushoto).

Comments