RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

"ACHENI KUUWA KARAMA ZA WATU ENYI WATUMISHI WA MUNGU MULIOSOMEA THEOLOJIA YA UTUMISHI", APOSTLE BASHANDO SHABOKA ALIFUNGUKA

Angel Lubala mtoto wa Mchungaji Deo Lubala aliwahi kushiriki mashindano ya Miss Tanzania, walokole mkaongea sana, mkahukumu sana na kuleta sheria zenu za kidini ambazo zinamnyima mtu uhuru wa Kristo. Sasa huwa najiuliza, hivi biblia zenu huwa mnazisoma vizuri au mnakariri tu mambo mliyofundishwa na wachungaji wa thiolojia?


Bishop Bashando Shaboka
Mnadhania kilichofanyika katika kitabu cha Esta kina tofauti gani na mashindano ya umiss?
Acheni kuua karama za watu kwa kudhania kila mtu ameitwa ili asimame madhabahuni kufundisha na kufukuza pepo. Tumeokolewa kwa neema na hata vipaji vyetu inabidi vimtangaze Kristo, kanisani kwangu ni ruksa hata mtu kuwa bondia au mcheza miereka, maana ktk historia ya Samsoni sijaona sehemu akihubiri wala kutoa pepo, yeye alikuwa mtu wa makarateka, anakupasua kweli tena kwa utukufu wa Mungu.

Lazima kanisa liproduce vipaji, tupate wacheza mpira waliookoka, ma actor wa bongo movie kama vile Peter Lusse na Uncle Jimmy, wanasheria wanaofuata nyendo za Nabii Yona na Nabii Isaya kama Pastor Justine Kaleb na Addo November Mwasongwe, Wanasiasa kama Daudi, Suleman, Yehoshafati etc. Wafugaji na wafanya biashara, wakulima kama Amosi ambo Edwin Seleli kafuata mkumbo huo. Sio wote tuishie ktk mtazamo mmoja wa kuwa manabii mitume na wachungaji, na akiinuka mwingine ambae anamtumikia Mungu ktk karama ya kutunisha misuri tunaanza kumshuku na kumuanzishia maneno ya chinichini. Big up sana Street Gospo Ministri aliyekuita ni Mungu na yeye ndio wa kukuhukumu.
Upendo Johnson kaza kamba, kupitia umodel huo huo utawaleta wengi kwa Kristo. Hakuna kukata tamaa kwa ajiri ya mapokeo ya kizee...

Comments