RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BAADA YA KUTIKISA JIJINI ARUSHA UPENDO KWA MAMA KUWASHA MOTO JIJINI DAR ES SALAAM


Upendo Kwa Mama baada ya kufanya vizuri sana jijini Arusha sasa wakazi wa jiji Dar es Salaam mmepata upendeleo wa kufanyika tamasha kubwa la kufungua mwaka la UPENDO KWA MAMA. Katiaka tamasha hilo kutakuwa na waimbaji mbalimbali kutoka Dar es Salaam na jijini Arusha wakijumuika pamoja kumtukuza Mungu kwa wema wake juu ya mama zetu waliotuzaa na waliotulea.

Katika tamasha hilo kutakuwa na mgeni Rasmi Mh. Mwigulu Lameck Nchemba Naibu Waziri wa Fedha na mgeni wa Heshima atakuwa Mh. Martha Mlata Mbunge wa Viti Maalum CCM Mkoa wa Singida.

Mh. Mwigulu Lameck Nchemba Naibu Waziri wa Fedha
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiSoMrJYdnnlwk5lwRTgUVWxytZV7BlBWL5Mh_5JRDDq1lAwac36tkbmGEzMhanvu6wRSl8K10GdCqlw3eEucnERl0bFjFOQryJRThTgZO4yatvMXIcHIReJ4rn2to5mumomH_-yvBQOWA/s1600/DSCN9474.JPG
Mh. Martha Mlata Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Singida.

Tunatambua ya kuwa mama ndiye mtu wa muhimu sana katika familia, mama ndiye aliyetutunza tangia tukiwa tumboni mwake, mama ndiye aliyetubeba na kuwa karibu sana nasi wakati tukiwa watoto, mama amevumilia mengi kutoka kwetu tukiwa watoto wenye usumbufu mwingi na kuna mambo mengi sana mama ameyafanya kuhakikisha unafikia kipindi unajitegemea.

Kwa kuona hivyo Upendo Kwa Mama Foundation ikiongozwa na Rais wake Eng. Carlos Mkundi ikaona ni vizuri kuwakumbuka akina mama na kuwaheshimu kwa upendo wao kwa kuwafanyia tamasha kubwa litakaloambatautoaji wa zawadi.




UPENDO KWA MAMA ILIVYOTIKISA JIJI LA ARUSHA MWAKA 2014

 Rais wa Upendo kwa Mama Foundation Eng. Carlos Mkundi
  Rais wa Upendo kwa Mama Foundation Eng. Carlos Mkundi
 Baadhi ya waimbaji walioimba siku hiyo
   Rais wa Upendo kwa Mama Foundation Eng. Carlos Mkundi
   Rais wa Upendo kwa Mama Foundation Eng. Carlos Mkundi

   Rais wa Upendo kwa Mama Foundation Eng. Carlos Mkundi


Comments