RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

MCHUNGAJI GODFREY MASSALU NA KAMATI YAKE WAELEZEA JUU YA MKESHA WA KULIOMBEA TAIFA LA TANZANIA KWA WAANDISHI WA HABARI

UONGOZI wa Fellowship Churches umekamilisha sehemu kubwa ya maandalizi kwa ajili ya Mkesha Mkubwa wa Kuliombea Taifa utakaofanyika tarehe 31 Desemba katika uwanja wa Taifa.

Akizungumza na wanahabari katika Ukumbi wa Habari Maelezo, mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya mkesha huo, Mchungaji Godfrey Mallassu alisema: ‘’Tamasha hili lina lengo la kuiombea amani nchi yetu na tunawaasa sana viongozi wa kisiasa wanaotaka madaraka kwa nguvu na kutumia nguvu za giza waache, wamtumikie Mungu kwani ndiye anayeweka viongozi madarakani.”


Mwenyekiti wa Kamati ya Maadalizi, Mchungaji Godfrey Mallassu, akizungumza na wanahabari (hawapo pichani).


Askofu Gama akisisitiza jambo.

Baadhi ya wanakamati kutoka kulia ni Mchungaji Derrick Luhende, Askofu Godfrey Mallassu, Askofu Gama na Mchungaji Olivia Mallonga.

Bango la Mkesha Mkubwa wa Taifa.
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa kwenye mkutano.

Comments