RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

MCHUNGAJI WA KANISA LA DCT RON SWAI AFURAHIA UWEPO WA VOICE OF TRIUMPH (VOT) KANISANI KWAKE

Mchungaji Ron Swai akiwa na furaha juu ya uwepo wa watoto wa Arachuga wanajiita Voice Of Triumph walivyoweza kumtukuza Mungu kanisani kwa Tabata Shule jijini Dar es Salaam. Kikundi hiki kiliweza kumaliza tour yake hapa jijini Dar es Salaam katika kanisa teule la Mungu la DCT kikiwa na furaha kutimiza moja ya ndoto yao.

Mungu wetu wa mbinguni anawatumia waimbaji hawa kwa kiwango cha juu sana, jamii imewakubali na mbingu naamini imewakubali kwa uimbaji wao wa kipekee sana ukilinganisha na waimbaji wengine. Waimbaji wenye kuonyesha bidii waimbapo na wenye shauku ya kumtumikia Mungu wetu.

Mchungaji kiongozi wa kanisa la DCT Tabata Shule Ron Swai wa pili kutoka kushoto

Rumafrica inampongeza sana Mchungaji Ron Swai na waumini wote wa kanisa la TAG - DCT kwa upendo na ukarimu wa kuwakaribisha wageni hawa kufanya huduma katika kanisa analoliongozana kuhitimisha tour yao ndani ya ntumba ya Bwana iliyojaa upako wa ajabu.


Kabala ya kuingia kwenye ibada Angel Benard a.k.a shemeji akipata kifungua kinywa.






























.









Picha na Uncle Jimmy

Comments