Marehemu Lihle Mbanjwa akiimba kwa hisia katika tour ya 17 ya kundi hilo, mwaka jana.
Majonzi yameigubika familia ya kundi maarufu la Joyous Celebration la nchini Afrika ya kusini, baada ya mwimbaji wao wa sauti ya kwanza mahiri wa muda mrefu aitwaye Lihle Mbanjwa kufariki dunia katika ajali mbaya ya gari binafsi waliyokuwa wakisafiria huku pia mpiga ngoma (drums) maarufu wa kundi hilo Siyabulela Satsha aliyekuwemo katika gari hilo akijeruhiwa kichwani na kulazwa hospitali.
Siyabulela akicharaza ngoma.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na kundi hilo, imesema ajali hiyo imetokea mapema siku ya jana jumapili, ambapo ndani ya gari hilo pia alikuwemo ndugu wa marehemu ambaye pia amelazwa hospitali pamoja na Sabu kwa matibabu zaidi.
Marehemu Lihle ambaye alifunga ndoa mapema mwaka huu na bwana Busie Shozi (Bonyeza hapa kuona harusi yake), alikuwa mmoja kati ya waimbaji nyota kwa upande wa sauti ya kwanza, hali iliyomfanya kushirikishwa katika kanda za waimbaji mbalimbali akiwemo malkia wa muziki wa injili Rebecca Malope, Ntokozo Mbambo, Nqubeko Mbatha na wengineo.
Mwimbaji huyo pia aliweza kuongoza wimbo katika rewind DVD ya 1 ya nyimbo za zamani za kundi hilo akiwa sambamba na mwanakaka Xolani Mdlalose, huku pia akianzisha wimbo katika DVD ya 15 part 1. Lihle alikuwa na urafiki wa karibu sana na waimbaji waliomaliza mkataba na Joyous akiwemo Duduzile, Mahalia, Ntokozo, Hlengiwe, Brenda ilifikia mpaka wakataka kuanzisha mfuko wa pamoja wa kuwasaidia watu wenye shida. Kundi hilo limepatwa na msiba ikiwa jumamosi walifanya onyesho huko Kimberley, wiki hii wakitarajiwa kuelekea nchini Swaziland kabla ya kuelekea nchini Kenya tarehe 14 kwa onyesho lingine.
Marehemu Lhile Mbanjwa wa kwanza kushoto mstari wa pili, akiimba kwa hisia katika onyesho lao la jumamosi iliyopita huko Kimberley Afrika ya kusini.
Marehemu Lihle akiwa na marafiki zake wa karibu ambao walishamaliza mkataba na Joyous, Mahalia, Dudu na Brenda Mtambo. walikuwa wakijiita Divas
Mahalia,Duduzile,Brenda,Hlengiwe na marehemu Lihle enzi za uhai wake.
Lihle akiwa na Ntokozo, Hlengiwe pamoja na Kuki ambao kwa pamoja wanaimba bendi ya Ntokozo na Nqubeko kama waitikiaji.
BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA JINA LA BWANA LIBARIKIWE
UKITAKA KUONA VIDEO ZAKE BONYEZA HAPA: Gospel Kitaa
Comments