UZINDUZI WA DVD YA SEMA NA YESU NA AUDIO CD YA MUNGU ANAWEZA YA TUMAINI NJOLE WAFANA KATIKA KANISA LA K.K.K.T SINZA KUMEKUCHA
Uzinduzi ambao ulionekana kukonga mioyo ya walio wengi waliofika katika kanisa la K.K.K.T Sinza Kumekucha hapa jijini Dar es Salaam ambapo mwimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania Tumaini Njole alipokuwa akizindua DVD yake ya Sema na Yesu na Audio CD yake ambayo ni toleo jipya (Vol.2) inayoitwa Mungu Anaweza.
Tumaini Njole akielekea madhabahuni kwaajili ya uzinduzi
Kitu kilichowashangaza wengi ni pale tu Tumaini alipokuwa akiingia madhabahuni kwa kuimba nyimbo za kuabudu ambazo ziliwagusa walio wengi na baadhi ya watu waliweza kutokwa na machozi. Hakika Tumaini Njole ni mwimbaji wa tofauti sana kiuimbaji na hata anavyoweza kucheza.
Tumaini Njole akiingia madhabahuni kwa kuimba nyimbo za kuabudu
Tamasha hili la uzinduzili lilihudhuriwa na waimbaji wengi sana kama utakavyowaona katika picha hapo chini. Na pia kulikuwa na viongozi kutoka serikalini kama Mh. Martha Mlata (Mbunge wa Viti Maalum (CCM) mkoani Singida ) ambaye aliweza alimuwakilisha mgeni rasmi, Mh. Mwigulu Lameck Nchemba ambaye alitakiwa kuwa mgeni rasmi wa tamasha hili.
Tumaini Njole
Kwa watu wasiomjua Tuamini Njole, huyu ni mwimbaji wa nyimbo za injili maarufu sana hapa nchini Tanzania, kipindi cha nyuma aliweza kuwa stage show malikia wa muziki wa injili Tanzania Rose Muhando kwa kipindi kirefu, lakini baadae mwenyezi Mungu aliweza kumpa karama ya uimbaji na kuwa mwimbaji wa kujitegemea.
Tumaini Njole
Tumaini Njole amekuwa nyota na asali kwa walio wengi kwani amekuwa akialikwa kwenye mikutano na matamasha mbalimbali kwa kazi ya Mungu na pia watumishi wa Mungu wamekuwa wakimtumia sana katika makongamano yao. Hii inatokana na jinsi mwimbaji huyu anavyojituma kufanya kazi ya Mungu na pengine kujinyima hata kufanya mambo yake na badala yake kutumia muda mwingi kwa kazi ya Mungu.
Tumaini Njole
Watu wengi wametokea kubarikiwa na kazi zake za uimbaji na inafika kipindi watu wanatamani hata kugusa mavazi yake wakati akiimba ili mradi tu wabarikiwe na zile nguvu za Mungu zilizomo ndani yake. Hakika tuna kila sababu ya kumshukuru Mungu kwa kutupa mwimbaji bora na mwenye bidii katika kuinua imani za watu kwa njia ya uimbaji.
Mbali na uimbaji, Tumaini Njole ni mwinjilisti mzuri sana, amekuwa akifanya kazi hii ya uinjilisti hasa pale anapopata bahati ya kuhudhuria baadhi ya mikutano iliyoandaliwa na watumishi wa Mungu. Kabla ya kuimba Tumaini Njole huanza kwa kutoa maneno mazuri sana kwa wapenzi wake kwa kuwafundishaNeno al Mungu.
Kuna mambo mengi yakuzungumza juu ya huyu mwimbaji Tumaini Njole, tutatafuta muda na utaweza kumsikia kwa kupitia RUMAFRICA Online TV.
Tumaini Njole
KIPINDI CHA KUKABIDHI RISALA KWA MGENI RASMI MH. MARTHA MLATA
Katibu Mwenezi wa Chama Cha Muziki Tanzania Stella Joel akimkabidhi mwakilishi wa mgeni rasmi, Mh. Martha Mlata ambaye pia ni mlezi wa chama hicho risala ya Tumaini Njole baada ya kusomwa
Mgeni Rasmi Mh. Martha (kulia) Mlata akihifadhi risala ya Tumaini Njole baada ya kuisoma
KIPINDI CHA KUZINDUA DVD NA AUDIO YA TUMAINI NJOLE
KIPINDI CHA KUZINDUA DVD NA AUDIO YA TUMAINI NJOLE
Mh. Martha Mlata akionge machache kabla ya kuanza zoezi la uzinduzi
Mchungaji wa kanisa hili la KKKT Sinza Kumekucha (kushoto) akiombea DVD na Audio CD ya Tumaini Njole na kiweka wakfu
Mh. Martha Mlata akionyesha Audio CD baada ya kukata utepe. Upande wa kulia ni mwimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania, Furaha Isaya
KIPINDI CHA KUNADI DVD NA AUDIO CD YA TUMAINI NJOLE
Baadhi ya wimbaji wa nyimbo za Injili waliojitokeza kununua DVD na Audio CD ya Tumaini Njole
Furaha Isaya (kushoto) akiwa ameshika DVD na Audio CD tayari kuwagawia waimbaji kumuunga mkono Tumaini Njole
Ndugu yake na Mh. Martha Mlata wa pili kutoka kulia akipokea DVD
Edson Mwasabwite akipokea Audio CD ya Tumani Njole kutoka kwa Furaha Isaya
Kutoka kushoto ni Leah, Upendo Nkone, Neema Mwaipopo na Mh. Martha Mlata, wote ni waimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania
Mch. Lucy Wilson akitoa ahadi yake ya kumchangia Tumaini Njole
Mwimbaji Lilian Kimola (kushoto) akimwandika jina Leah baada ya kuahidi kumchangia Tumani Njole
Mwimbaji Lilian Kimola (kushoto) akimwandika jina Leah baada ya kuahidi kumchangia Tumani Njole
BAADHI YA WAIMBAJIWA NYIMBO ZA INJILI WALIOMBEA
Madam Ruti
Silas Mbise (mwenye suti)
Upendo Nkone (kushoto) na Mh. Martha Mlata
Judy Sanga (kushoto) na Jessica Sanga wa pili kutoka kushoto
Mh. Martha Mlata akimtunza Upendo Nkone wakati akiimba
Ammy Mwakitalu wa tatu kutoka kulia akimuimbia Mungu wake
Edson Mwasabwite alivyoweza kuwa moto katika tamasha la Tumaini Njole
ANGALIA MATUKIO MENGINE KWA KUBONYEZA "READ MORE" HAPO CHINI KIDOGO
MATUKIO MENGINE YALIYOTOKEA KATIKA TAMASHA LA TUMAINI NJOLE
Comments