RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

EXCLUSIVE: FRIDA FELIX TISHIO KWA UIMBAJI WAKE NA SAUTI YAKE. AWEKA HADHARANI HISTORIA YA MAISHA YAKE KIMUZIKI

Mwanasheria na mwimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania Frida Felix kwa mara ya kwanza aliweza kutua katika ofisi ya Rumafrica baada ya kupata mwaliko na utawala wa ofisi hiyo. Ujio wake ulikuwa ni kwaajili ya kutaka kujua historia fupi ya maisha yake kimuziki. Katika clip hii kuna mambo mengi sana aliweza kuyaeleza ambayo wewe ukiyasikiliza yatakusaidia sana.

Frida Felix
Frida Felix kwa asilia anatokea Songea ila maisha yake yote yuko Dar es Salaama, na kwa sasa akichukua stashahada (degree) yake ya Uanasheria katika chuo kilichopo maeneo ya Ubungo katika Jengo la Mawasiliano Tower. Huduma yake ya uimbaji ilianza mara tu alipopata ufahamu kuwa anaweza kumtumikia Mungu kwa njia ya uimbaji nikimaanisha akiwa mdogo sana.

Frida Felix
Frida Felix amezaliwa katika familia ya Wakristo na amekuwa akiishi maisha ya Ukristo tangia akiwa mdogo mpaka sasa yuko ndani ya Ukristo akimtumikia Mungu. Katika maisha yake ya Ukristo amesema kuna mambo mengi ameyaona yakifanyika katika maisha yake na mpaka leo anaitwa Mwimbaji Frida, na ndio maana anazidi kumtukuza huyu Mungu wetu kwasababu anamtendea yaliyo mema katika maisha yake.

Frida Felix
Mwimbaji huyu mbali na uimbaji wake pia ana ndoto kubwa sana kuwa mwigizaji wa kimataifa, hii ni kutokana na kutambua kipaji chake hiki akiwa mdogo sana, ameshawahi kufanya uigizaji akiwa shuleni na alikubalika sana na walimu wake na wanafunzi wake kwa uigizaji mzuri. Mwimbaji huyu ni mwimbaji wa kipekee sana ukikutana naye na kuongea naye, hasa alivyo na heshima na utii.

Malengo yake ya sasa ni kumalizia albamu yake ambayo bado iko jikoni. Akiongea na Rumafrica amesema anaamini kwa asilimia 100 ujumbe aliopewa na Mungu utafanyika tiba katika maisha yako kama utausikia na kuufanyia kazi.

Frida Felix

Nisikumalizie uhondo wa historia ya maisha ya mwimbaji huyu mahili Tanzania na Afrika nzima, sasa ninaomba umsikilize akiimba na akielezea historia ya maisha yake.

Comments