RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

ODAMA AMSHUKURU MUNGU KWA USHINDI ALIOPATA - REDIO UHURU 95.7 FM

Picha zimepigwa na Rumafrica +255 715 851523
Rumafrica siku ya leo ilishuhudia mahojiano yaliyofanyika katika kituo cha redio Uhuru Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam katika kipindi cha FILAMU ZETU kinachoendeshwa na Mama Abdul juu ya ushindi aliopata mwigizaji wa filamu na mkurugenzi wa J-Film 4 Life, Jeniffer Kyaka (Odama) alimshukuru sana Mungu kwa ushindi aliopata baada ya kushindanishwa kati yake na mwigizaji mwenzake Irene Paul kumtafuta mwigizaji bora.

Jeniffer Kyaka (Odama)

Odama alisema, watu wanaweza kuona ni kitu kidogo sana, lakini yeye anakithamini sana kwani kwake ni faraja kubwa sana kuona kuna watu wanahangaika kwaajili yake. Watu wanatumia muda wake na pesa zao kupiga simu redioni kunizungmzia na haitoshi wanaamua kunipigia simu ili nishinde. Nawashukuru sana wadau wangu.

Kipindi hicho kilikuwa kinapambanisha waigizaji bora Tanzania ambapo Odama alipambanishwa na mwigizaji mwenzake Irene Paul. Wasikilizaji wa redio Uhuru waliweza kupiga simu na wengine kutuma meseja za kupiga kura kwa yule msanii waliona ni bora kwao. Hatiamye Jeniffer Kyaka (Odama) aliweza kuchukua ushindi
Mtangazaji wa Redio Uhuru katika kipindi cha filamu Zetu Mama Abdul (kushoto) akisoma historia ya msaanii wa filamu nchini Kenya, na kulia ni Odama akifuatilia historia hiyo.

Odama alimshukuru Mungu kwa ushindi alioupata na pia kwa wale wote waliompigia kura kwa njia ya simu. Ni kitu ambacho hakutegemea kabisa kuwa ataibuka mshindi wa shindano hilo kabambe. Aliwashukuru sana watangazaji wa redio hiyo na uongozi mzima kwa kumpa heshima ya kufanya mpambano huu mkali. Radio Uhuru ni moja ya redio bora Tanzania kwa kazi za wasanii na ndio maana wameamua kuanzisha kipindi cha Filamu Zetu.
 Odama na mmoja wa watangazaji wa kipindi cha Filamu Zetu
Wadau waliweza kuuuliza maswali juu ya malengo yake ya baadae, naye Odama aliweza kufunguka na kuwaeleza kwa sasa yuko katika maandalizi ya kufungua kituo kwaajili ya kuinua vipaji vya wasanii wadogo ili waweze kujulikana kama yeye alivyojulikana na jamii ya Tanzania
 Mama Abdul (kushoto) na Jeniffer Kyaka (Odama)
Wengine walitaka kujua idadi ya filamu ambazo amecheza, naye alisema mpaka sasa amecheza filamu zaidi ya 20 na hivi sasa ametoa filamu mpya inayoenda kwa jina la JADA ambayo itakuwa sokoni tarehe 19.02.2015 kwahiyo wadau wakae mkao wa kula kujipatia filamu mpya. Katika filamu hiyo wataweza kuona mtoto anayeishi na mama wa kambo anavyosumbua familia na kusababisha malumbano na kuvunjika kwa amani ndani ya familia.
 Baadhi ya wadau walitaka kujua siri kubwa ya Odama kutokuwa na skendo mbaya kama baadhi ya wasanii wenzake, naye alisema, hii ni kutokana na jinsi yeye alivyojiwekea katika maisha yake kuwa atajitahidi sana kuishi kama Jeniffer Kyaka na sio kuishi yale maisha ambayo anaigiza katika filamu. Hii imemsaidia sana Odama na ndio maana mpaka leo jamii inamtambua Odama kama mwigizaji asiye na skendo. Pia malezi aliyolelewa na wazazi wake ambayo ni wacha Mungu na hapendi kuona anawaangusha wazazi wake kwa skendo.
Wadau waliweza kupiga maswali mengi sana na hasa juu ya waigizaji wa filamu kuvaa mavazi ya ajabu katika jamii inayowazunguka kama wanavyofanya katika filamu zao, naye Odama alisema, hiyo ni tabia ya mtu na sio kitu kingine, kama mtu amezoea tabia hiyo ataendelea kuwa hivyo. Pia aliwaomba watu wasiwachukulie wasanii kama wote wana tabia mbaya kutokana na wanavyoona katika filamu zao bali watambue ya kuwa kile wanachofanya ni kuwakilisha vitu vinavyotokea katika maisha ya watu mitaani.

 Mkurungenzi wa Rumafrica, RuleaSanga (kulia) na mtangazi wa kipindi cha nyimbo za tarabu redio Uhuru
 Mkurungenzi wa J-Film 4 Life, Jeniffer Kyaka -Odama (kushoto) na Kaimu Mkurugenzi wa redio Uhuru, Angel A. Akilimali (kulia)
 Kaimu Mkurugenzi wa redio Uhuru, Angel A. Akilimali
  Mkurungenzi wa J-Film 4 Life, Jeniffer Kyaka -Odama
 Mkurungenzi wa J-Film 4 Life, Jeniffer Kyaka -Odama (kushoto) akikabidhiwa zawadi ya kalenda ya CCM na Kaimu Mkurugenzi wa redio Uhuru, Angel A. Akilimali (kulia)

ULIFIKA WAKATI WA KUPIGA PICHA ZA PAMOJA
Baadi ya wafanyakazi na watangazaji wa redio Uhuru waliweza kupiga picha za kumbukumbu na Odama na ilikuwa kama hivi"-

 Mtangazaji wa redio Uhuru kipindi cha Burudani Ambiance Shtuka, Cecy Jerry aka Mama Cecy au Mwasii Kitoko (kushoto) akiwa na Jeniffer Kyaka (Odama)
 Mtangazaji wa redio Uhuru Scolastica Salim (kulia) akiwa na Odama
 Mtangazaji Neema Mwangomo (kulia) na Jennifer Kyaka (Odama)
  Mtangazaji Neema Mwangomo (kulia) na Jennifer Kyaka (Odama)
 Mtangazaji wa redio Uhuru kipindi cha Hello Tanzania, Sheila Simba (kulia)  na Jennifer Kyaka (Odama)
  Mtangazaji wa redio Uhuru kipindi cha Hello Tanzania, Sheila Simba (kulia) na Jennifer Kyaka (Odama)

Comments