RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

KANISA LA MCHUNGAJI JOSEPHAT GWAJIMA KAWE LATAKIWA KUVUNJWA


Mchungaji Mchungaji Josephat Gwajima

Nakala ya barua kutoka kwa Meneja wa Mkoa wa Kinondoni wa NHC.

KANISA la Mchungaji Josephat Gwajima lililokuwa likiendesha shughuli katika viwanja vya Tanganyika Packers Kawe, wilaya ya Kinondoni, jijinI Dar limeamriwa kuondoka eneo hilo.

Kanisa hilo ambalo kwa muda mrefu limekuwa likiendesha shughuli zake eneo hilo limedaiwa kusababisha usumbufu na kero kubwa za makelele kwa wakazi wa maeneo hayo.

Barua iliyosainiwa na Meneja wa Mkoa wa Kinondoni wa Shirika la Nyumba la Taifa, B.N. Masika, imesisitiza kwamba pamoja na kutambuliwa umuhimu wa kanisa hilo kuendesha shughuli zake shirika hilo halitaweza kutoa ruhusa kwa kanisa hilo kuendelea kufanya mahubiri katika viwanja hivyo,kwani shirika hilo limeshaanza kutumia viwanja hivyo kwa maendeleo ya wananchi wa Kawe ikiwa ni ujenzi wa makazi n.k

Barua hiyo imetoa 30 zinazoishia tarehe 9 Machi mwaka huu ili Mchungaji Gwajima ajitayarishe kuondoka eneo hilo.

Comments