RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

KAZI YA MUNGU INAONEKANA KWA WAKAZI WA KIBAHA BAADA YA MTUME NYAGA KUWASHA MOTO WA INJILI UNAOENDELEA HIVI SASA

Kama wewe hutahubiri Injili, Mungu anao wengi wa kufanya kazi yake. Hivi sasa anamtumia Mtume Peter Nyaga wa kanisa la RGC Tabata Chang'ombe lililopo jijini Dar es Salaam Tanzania, kupeleka habari Mungu kwa wakazi wa Kibaha - Dar es Salaam. Watu wanamiminika kama maji katika mkutano huo kupokea majibu yao na kupata Neno la Mungu kwaajili ya kuinua IMANI zao ili wazidi kudumu katika wokovu. Mtume Peter Nyaga akiwa na mwenyeji wake Bishop Dr. Grevase Masanja wamejipanga kwa kazi ya Mungu na kuvuruga kazi za shetani.

Kongamano hili la Urejesho linarejesha vile vilivyopotea na adui shetani  na kukusababishia matatizo katika maisha yako, umeachwa mtupu na ukisongwa na mawazo mengi, shida zimekuwa ni moja katika maiasha yako.

Unachotakiwa sasa ni kufika katika kongamano hili la kipekee ili upate ujumbe na mwisho wa siku kupokea baraka zako. Waimbaji kama Atosha Kissava, Tumaini Njole na Upendo Nkone wamejipanga kushusha wingu la uwepo wa Mungu kwa njia ya uimbaji.

Sasa, kutokwenda kwako kwenye kongamano ni hasara yako na sio ya mtume wala waimbaji, kama hutaenda wapo waotakaoenda wenye nia ya kupokea ujumbe kutoka kwa Mungu kwa kupitia watumishi wako.

 MAMBO YANAVYOENDELEA KIBAHA NA MTUME PETER NYAGA





Comments