RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

MATUKIO YA TAMASHA LA BARAKA MWAIJANDE KATIKA KANISA LA K.K.K.T MBEZI LOUS DAR ES SALAAM

Baraka Mwaijande kwa neema na huruma ya Mungu aliweza kufanikisha lile lengo lake alilolipanga kukamilisha suala lake la uzinduzi wa albamu yake ya "Sema Nami Bwana" katika kanisa la KKKT Mbezi lous jijini Dar es Salaam.

Tunamashukuru sana Mungu kwa wema wake, kwani watu wengi walijitokeza kumuunga mkono mtumishi huyu wa Mungu. Waimbaji mbalimbali waliweza kufika na kuhakikisha kazi ya Bwana inasonga mbele.

Sasa ni kazi kwako na mimi kutafuta DVD ya Sema Nami Bwana ili uweze kupata ujumbe wa Mungu kupitia uimbaji wa Baraka Mwaijande. Kuna kitu ambacho Mungu amemjalia Baraka kwaajili yako na njia peke ya kupata ni kujipatia DVD hii. Ni vigumu sana Baraka kupita kwa kila mtu na kumhubiria ila kwa njia ya DVD yake utaweza kupata ujumbe wa Bwana.

Baraka Mwaijannde kwa kupitia mitandao mbalimbali aliweza kumshukuru sa Mungu na kuwashukuru watu wote walioshirikiana naye katika maandalizi ya tamasha lake na pia wale wote waliofika katika tamasha hili la kihistoria.Baraka Mwaijande akiimba siku ya tamasha
 Kulia ni Mc Joshua Makondeko na anayefuatia ni Mgeni rasmi
 Baraka Mwaijande (kushoto) akiwa na muwakilishi wa mgeni rasmi

 Mc Joshua Makondeko akihamasisha watu

Edson Mwasabwite (kushoto) na Emmanuel Mbasha (kulia)

Tangazo limetengezwa na Rumafrica +255 715 851 523

Comments