RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA CHEMSHA BONGO NA BIBLE SEHEMU YA PILI

Tunawashukuru sana watumishi wa Mungu kwa ushirikiano wenu kwa kujibu maswali ya Chemsha Bongo na Bible, leo tunakuomba ujibu haya maswali. Huruhusiwe kuangalia majibu kabla hujajibu, Roho Mtakatifu ndio msimamizi wako



KITABU CHA LUKA

MASWALI


  1. (a) Mwezi wa sita Mungu alimtumia Malaika Gabriel kwenda mpaka mji wa Galilaya, jina lake Nazareti kwa mwanamwali bikira aliyekuwa amepozwa na mtu, jina lake Yusufu, na huyo bikira jina lake Mariam. Malaika Gabriel alipoingia nyumbani kwake, alimwambia nini?

    (b)  Ni maneno gani malaika Gabriel alimjibu Elizabeti baada ya kuona amestajabishwa moyoni mwake baada ya kupokea salamu kutoka kwa malaika Gabriel ambayo hiyo salamu hakujua maana yake?

    (c) Ni kitu gani Malaika Gabriel  alimwimbia Elizabeti kuhusiana na mamlaka aliyokuwa nayo Yesu baada ya kuzaliwa kwake?

  2. Malaika alipomuuliza Malaika Gabriel yakuwa itakuwaje kuhusiana namimba wakati hamjui mume?

  3. (a) Kichanga cha Elizabeti mke wa kuhani Zakaria kilifanya nini tumboni mwa mama yake, baada ya Mariamu kusalimiana na Elizabeti?

    (b) Ni kitu gani kilimtokea Elizabetibaada ya kichanga kuruka ndani ya tumbo lake?

    (c) Mariamu alikaa na Elizabeti kwa muda gani kabla hajarudi nyumbani kwake?

  4. (a) Mtoto wa Elizabeti alitahiriwa siku ya ngapi?

    (b) Ni jina gani walitaka kumpa motto wa Elizabeti?

    (c) Elizabeti alikubaliana na jina la mwanae kuitwa zakaria? Kama hapana jina gani alimpa?

    (d) Je, watu walikubali motto wa Elizabeti kuitwa Yohana? Kama hapana
               (i) Kwanini walikataa?
               (ii) Walifanyeje kupata jina halisi?

    (e)  Nini kilimtokea Zakaria ambaye alikuwa haongei baada ya kuandika jina la motto wake katika kibao?

MAJIBU

  1. (a) Salamu uliyepewa neema, Bwana yu pamoja nawe, Usiogope (Luka 1:28)

    (b)  Usiogope, Mariamu kwa maana umepata neema kwa Mungu, Tazama utachukua mimba na kuzaa mwanaume na jina lake utamwita Yesu (Luka 1:22)

    (c) Alimwambia
             (i) Yesu ataitwa mwana Aliye juu
             (ii) Bwana Mungu atampa kiti cha enzi cha Daudi, baba yake
             (iii) Atamiliki nyumba ya Yakobohata milele
             (iv) Ufalme wake hatakuwa na mwisho
              (Luka1:32-33)

  2. Malaika akamwambia, Roho Mtakatifu atakuujia juu yako, na nguvu zake zitakufunika kama kivuli, kwasababu hicho kitakachozaliwa kitakuwa kitakatifu, Mwana wa Mungu (Lika 1:35)

  3. (a) Kitoto kichanga kiliruka ndani ya tumbo lake (Luka 1:41)

    (b) Elizabeti alijazwa na Roho Mtakatifu, akapaza sauti kwa nguvu, akasema, Umebarikiwa wewe katika wanawake wote, naye mzawa wa tumbo lako amebarikiwa (Luka 1:41-42)

    (c) Muda wa miezi mitatu (Luka 1:56)

4. (a) Siku ya nane (Luka 1:59)

    (b) Jina la baba yake la Zakaria (Luka 1:60)

   (c) Hapana, bali alimpa jina la Yohana (Luka 1:60)

   (d) (i) Hawakukubali kuitwa Yohana kwasababu katika jamii yao hakuna mtu anaitwa hivyo

        (ii) Wakamwashiria baba yake wajue atakavyomwita Zakaria akataka kibao na kuandika jina lake kuwa Yohana Luka 1:61-63)

(e) Kinywa chake kilifunguliwa na ulimi wake pia, akaanza kunena akisifu Mungu (Luka 1:64) na akajazwa na Roho Mtakatifu (Luka 1:67)


Maswali yameandaliwa na Rumafrica
+255 715 851 523

Comments