RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA YAFOTOA MAPICHA YA ODAMA NA MTANGAZAJI WA ITV GODWIN GONDWE KATIKA STUDIO ZA TBC (KIPINDI CHA ULIMWENGU WA FILAMU) NA KATIKA OFISI YA RUMAFRICA

Picha  na  Habari: Rumafrica
Siku ya alhamisi 13.02.2015 Mkurugenzi wa kampuni ya J-Film 4 Life na mwigizaji wa filamu nchini Tanzania, Jennifer Kyaka (Odama) aliweza kualikwa katika kituo bora cha utangazaji cha TBC1 kwajili ya kuelezea ujio wa filamu yake mpya ya JADA ambayo inategemea kutoka Feb.19.2015. Akifanya mahojiano na mtangazaji ambaye ametokewa kupendwa na wapenzi wengi wa filamu duniani, Bwana Juma ambaye anatangaza katika kipindi cha Ulimwengu wa Filamu, aliweza pia kuelezea historia fupi ya maisha yake.
Kutoka kulia ni mtangazaji wa Ulimwengu wa Filamu, Juma akifuatiwa na Jennifer Kyaka (Odama)

Mahojiano hayo yaliyochukua muda mrefu, Odama aliweza kuelezea kidogo kuhusiana na filamu JADA na kusema, katika filamu hiyo kuna mtoto ambaye anaitwa Jada ambaye anaishi na mama yake wa kambo pamoja na baba yake. Mtoto huyu ambaye anatabia ya kumdharau mama yake wa kambo na kumuona hana kitu, anaamua kuanza kufanya vituko ndani ya nyumba ili baba yake aweze kumuona mke wake ambaye ni mama yake wa kambo wa Jada kuwa hafai. Jada anajitahidi na inafikia kiasi anamshirikisha bibi yake ili aweza kutambua kuwa mama yake wa kambo (Odama) ni mkorofi.
Mbali na kuelezea ujio wa filamu yake ya JADA aliweza kuwaomba wadau waweze kunjipatia nakala yao ya DVD ya Jada ili waweze kuelimika na kile walichokicheza katika filamu hiyo. Filmau hiyo ambayo imeongozwa na Lamata, amesema hakika watu wataweza kujua kuwa hapa Tanzania tuna watunzi wa filamu wazuri ikiwa ni pamoja na waongozaji wa filamu wazuri. J-Film 4 Life ni kampuni ya Jennifer Kyaka, na ni kampuni ambayo inatengeneza kazi zote za Odama ambazo tumekuwa tukizangali sana.
Ulimwengu wa Filamu Crew walizeza kumfanyia surprise (sapraizi) Jennifer Kyaka (Odama) kwa kuwaleta mashabiki wake ambao wanampenda sana Odama ili waweze kumuona akifanya mahojiano katika kipindi pendwa cha TBC1 Ulimwengu wa Filamu
 Waliosimama (kulia ni Neema Minja) ni baadhi ya mashabiki waliomiminika kumuona Odama




 Mtangazaji wa ITV Bwana Godwin Gondwe na Odama ndani ya Rumafrica


  BAADA YA MAHOJIANO KUMALIZIKA, PICHA ZA PAMOJA ZILIFUATAZO

Mkurugenzi wa Rumafrica, Rulea Sanga (wa pili kutoka kulia)

ANGALIA PICHA ZINGINE KWA KUBONYEZA READ MORE HAPO CHINI










 Odama (kulia) akiwa na mdau wa Odama
















Comments