RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

UPENDO BENSON: TUSHIRIKIANE TABASAMU SIKU YA LEO

Upendo Benson

Nataka kushare tabasamu na marafiki zangu wote, yawezekana uko katika wakati mgumu, au una hasira au mtu amekukwaza, au unaumwa au unalia nk.. pia inawezekana hiyo kazi unayoifanya ni ngumu, au huipendi lakini inabidi ufanye kwasababu huna option nyingine, au una mazingira magumu ya kazi n.k.. pi inawezekana una maisha safi, au maisha duni, au upo nyumbani huna kazi, au biashara yako haiko poa nk.. unatakiwa kujua kwamba yote haya ni sehemu ya maisha, na mshukuru Mungu kwa kila jambo. Sasa, popote utakapoiona picha hii, changia kwa kutupia picha yako ukiwa na familia, mke/mume/watoto/wazazi/ndugu...ya muda huo ukiwa unatabasamu au unacheka bila kujali hali uliyonayo.. hata kama tabasamu haliji, fanya mazoezi ya kutabasamu/kucheka mpaka uweze.. usiogope wala usione aibu kushare tabasamu na kila siku ujizoeshe kutabasamu mpaka iwe sehemu ya maisha yako, maana inawezekana kutabasamu kwako kukambadilisha mtu na kumpa sababu ya kutabasamu..
TUSAHAU TOFAUTI ZETU, SHARE TABASAMU!!

Comments