BAADHI YA WANA USHINDI WASHIRIKI MSIBA WA SETH (KAKA YAKE NA MWANAUSHINDI ENOCE LAZARO)

Chama cha kusaidia cha USHINDI kiliweza kufika katika msiba marehemu Seth ambaye ni kaka yake na mwanaushindi Enoce Lazaro ambao ulifanyika nyumbani kwao Mabibo Lerini jijin Dar es Salaam Tanzania siku ya Jumapili 15/03/2014. Kikundi hiki ambacho malengo yao makuu ni kusaidia wakati wa shida na raha kwa waimbaji, wachungaji, wafanyakazi, wajasiriamali na mtu yeyote yule mwenye hofu ya Mungu. Kikundi hiki kilitoa pole kwa wafiwa, ndugu na jamaa wa marehemu waliofika katika msiba na wale ambao hawakuweza kufika katika msiba kwa njia moja au nyingine.

Mwanaushindi Enoce Lazaro ni muumini wa kanisa la Mito ya Baraka kwa Askofu Mwakiborwa na pia ni mwimbaji wa nyimbo za Injili na amekuwa akifanya kazi na Masanja Mkandamizaji katika kampuni ya ulinzi ya OK Security kama meneja masoko iliyopo hapa jijini Dar es Salaam - Tanzania. Sasa basi kama ungependa kutoa rambirambi yako waweza kumtumia kwa kupitia simu yake hii ya mkononi +255 712 152 552

Mwimbaji wa nyimbo za Injili na dancer wa Masanja Mkandamizaji, Enoce Lazaro aliyefiwa na kaka yake Seth
Baadhi ya waumini wa Kanisa la Mito ya Baraka

 Emmanuel Mabisa (kushoto) na Grace Wangwe
Kutoka kulia ni Elice Wangwe (mke wa George Lyanga), George Lyanga, mfiwa Enoce Lazaro.
0