RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA CHEMSHA BONGO NA BIBLE

 CHANZO: Maswali yanatoka Luka 20 hadi Luka 24

ONYO: Hurusiwi kuangalizia katika Biblia au kujibu kwa kuangalia majinu hayo hapo chini. Msimamizi wa huu mtihani na Yesu Kristo



Glorymainah-Mwimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania

MASWALI
  1. a) Yesu alipoinua macho yake juu akawaona matajiri wakitia sadaka zao katika sanduku la Hazina. Mjane aliyemuona Yesu akitia sadaka, alitia senti ngapi?

    b) Yesu alisema nini kwa mjane aliyetia sadaka kiasi kidogo?

    c) Yesu alisema nini juu ya watu kadha wa kadha walipokuwa wakiongea habari za hekalu jinsi lilivyopambwa kwamawe mazuri na sadaka za watu?

    d) Kwanini Yesu alisema, "Angalieni msije mkadanganyika, kwasababu wengi watakuja kwa jina langu wakisema mimi ndiye tena, majira yamekaribia"

    e) Taja ishara ambazo Yesu aliwambia watu juu ya siku za mwisho za hekalu lao zuri lililojengwa na kupambwa na mawe mazuri kubomoshwa

    f) Yesu aliwapa maneno gani yakuwatia moyo wale watu ambao hekalu lao zuri litakapoenda kubomoshwa?

    g) Yesu alisema nini kwa watu  juu ya ishara zitakapokuwa zimeanza kipindi cha hekalu zuri la mawe litakapo bomoshwa?
  2.  Malizia maneno haya ya Yesu kwa watu wake
    a) Basi jiangalieni mioyo yenu, isije ikaelemewa na .................................................
    b) Basi kesheni ninyi kila wakati mkiomba ili..............................................................
  3. a) Baada ya Yesu kufundisha wanafunzi wake alikuwa akienda katika mlima gani?
    b) Taja jina la sikukuu ya mikate isiyotiwa chachu
    c) Taja jina la mwananfunzi wa Yesu aliyeingiwa na shetani?
    d) Walimuahidi nini Yuda Iskariote juu ya kukamatwa kwa Yesu Kristo ili ateswe?
    e) Ni sehemu gani Yesu alitaka aandaliwe Pasaka?
    f) Yesu alitamka maneno gani alipotwa kikombe chake kipindi cha Pasaka akiwa na wanafunzi wake  na yule mwanaume aliyewakaribisha katika chumba chake cha ghorofani kufanyia sikukuu ya Pasaka?
MAJIBU
  1. a) Mbili
    b) Hakina ninawaambia, huyu mjane ametia zaidi kuliko wote, maana hao walitia sadaka, katika umaskini wake ametia vyote alivyokuwa navyo

    c) Haya mnayoyatazama, siku zitakuja ambapo halitasalia jiwe ambalo halitabomoshwa.

    d) Kwasababu watu walitaka kujua ishara za mawe ya hekalu lao zuri kubomoshwa na muda wa tukio hilo kutokea
    e) i. Taifa litaondoka kupigana na Taifa
        ii. Ufalme kupigana na Ufalme
        iii. Matetemeko makubwa ya nchi
        iv. Njaa ya tauni mahali mahali
         v. Mambo ya kutisha
       vi. Ishara Kuu kutoka Mbinguni
       vii. Watawakamata na kuwaudhi
       viii. Watawapeleka mbele ya Masinagogi na kuwaua magerezani n.k
    f) Basi mambo hayo yatakapotokeachangamkeni, mkaviinue vichwa vyenu kwa kuwa ukombozi wenu umekaribia
    g) Changamkeni mkaviinue vichwa vyenu kwa kuwa ukombozi wenu umekaribia
  2. a) Ulafi, na ulevi, masumbufu ya maisha haya
    b) mpate kuokoka katika haya yote yatakayowatokea na kusimama mbele za mwana wa Adam
  3. a) Mizeituni
    b) Pasaka
    c) Yuda Iskarioti
    d) Kumpa fedha
    e) Katika chumba cha ghorofa ya mwanaume aliyekutwa amejitwika mtungi wa maji
    f) Alishukuru akisema, Twaeni hiki  mgawanywe  nyinyi kwa nyinyi, maana nawambia ya kwamba tangu sasa sinywi mazao ya zabibu hata ufalme wa Mungu.

Comments